Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma imeridhishwa na maendeleo ya miradi ya ujenzi katikati shule ya secondari Mpitimbi mnamo tarehe 9 Octoba 2023 wakati wa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na ilani ya Chama cha Mapinduzi katika Mkoa wa Ruvuma.
Kamati hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma Mhe. Odo Mwisho waliweza kukagua ujenzi wa vyumba 9 vya madarasa, vyoo matundu 14 na mabweni 4 ambayo fedha zake zimetoka Serikali kuu kwa awamu mbili chini ya Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan
Akikagia miradi hiyo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma amewaomba wadau mbalimbali wa Chama na serikali kuwa na Imani na Chama cha Mapinduzi na kuendelea kumshika mkono Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa kwa kusimamia vyema fedha za miradi anazozitoa. Amesema
"Raisi wetu mama yetu mpendwa anahangaika huku na huku kutafuta fedha ili kuhakikisha mambo yanakwenda vizuri ndio maana amekubali kutoa fedha za kutosha kujenga miradi hii katika shule hii ya Mpitimbi na sisi kama Kamati ya siasa ya Mkoa wa tumeridhishwa na mwendo mzuri pamoja na ubora wa ujenzi katika shule hii Rai yangu kwenu ni kuhakikisha miradi hii inatumika vizuri ili iweze kudumu kwa muda mrefu, pia nichukue fursa hii kuwaambia ninyi mlioko hapa tuendelee kuwa na Imani na Raisi wetu"
"Tumeona Madarasa yale tisa sehemu nyingine hakuna marumaru lakini nyinyi mmeweka safi kabisa Lakini pia madawati safi na mmeweka umeme kwakweli mnnastahili pongezi Lakini kitu kukubwa ambacho nampongeza Mkuu wa shule ya secondari Mpitimbi ujenzi wake unakwenda kwa wakati na kama tulivyosikia hapa kwenye taarifa tuliyo somewa anatarajia kukamilisha kabla ya muda aliopewa, lakini tumeona ujenzi ambao umestahili viwango vyote maana tumepita sehemu nyingine huko hawajafikia hatua kama hii lakini ni miradi inayofanana na hii lakini hapa ubora tumeuona na unaridhisha, na ametuambia baada ya ujenzi huu kukamilika atabakiwa na akiba jambo ambalo mkuu wa shule anastahili pongezi kubwa sana"
Vilevile napenda kutoa Shukrani kwa Mhe Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuona umuhimu wa Elimu bora kwa watoto wetu na kuamua kutoa fedha hizo kujenga miundombinu hii ya kisasa katika shule hii, pia Shukrani zimfikie Mbunge wa Jimbo la Peramiho Jenista Joakim Mhagama kwa ufuatiliaji mzuri wa maendeleo ya Jimbo lake, pia Mwenyekiti wa Halmashuri, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Songea na timu yake kwa ujumla, Balaza la Madiwani na viongozi wote wa Chama Cha Mapinduzi kuanzia ngazi ya Kijiji mpaka Mkoa kwa kuhakikisha ilani ya Chama cha Mapinduzi inatekelezwa vyema.
Mkuu wa shule ya sekondari Mpitimbi akisoma taarifa ya fedha zilizopokelewa kwaajili ya utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu katika shule ya sekondari Mpitimbi amesema walipokea jumla ya shilingi 879,800,000.00, kwaajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa9, mabweni 5 na matundu ya vyoo14, kutoka Serikali Kuu na SEQUIP. Na Hadi sasa Madarasa 6 yamekamilika na yanatumika na 3 hatua ya ukamilishaji, huku matundu 14 ya vyoo yamekamilika, pia bweni 1 limekamilika na linatumika na 3 yapo katika hatua ya ukamilishaji.
Nae aliweza kutoa Shukrani kwa Mhe Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwapa fedha hizo ili kujenga miundombinu ya kisasa, pia, Mbunge wa Jimbo la Peramiho Jenista Joakim Mhagama kwa msaada wake wa hali na mali, pia Chama cha Mapinduzi kuanzia ngazi ya Kata hadi Mkoa kwa ufuatiliaji mzuri wa miradi hii pia Diwani wetu kwa kushirikiana nasi bega kwa bega na kamati nzima ya ujenzi kwa kuhakikisha mradi huu unakamilika.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa