Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango, iliyoongozwa na Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mhe Simon Kapinga, imempongeza Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mpitimbi kwa usimamiz mzuri wa miradi ya maendeleo katika eneo lake la kazi
Pongezi hizo zimetoleo leo tarehe 16.04.2024 wakati kamati hiyo ilipopita katika shule ya hiyo na kukagua ujenzi wa bweni jipya la wasichana lililopo ndani ya Shule hiyo.
“ Shule ya Sekondari Mpitimbi ni miongoni mwa shule za Sekondari zinazotekeleza mpando wa shule salama chini ya SEQUIP, hivyo ilipokea kiasi cha Shilingi 128,000,000/= (milioni miamoja ishirini na nane tu) mnamo tarehe12.04.2023 kwa ajili ya ujenzi wa bweni moja pamoja na miundombinu yake ( Vitanda)
Ujenzi ulianza rasmi mnamo tarehe 04.10.2023 na matarajio yetu ilikua kumaliza mnamo tarehe 04. 01. 2024 lakini kutoka na changamoto zimepelekea mradi kufikia hapa hadi sasa ila tupo kaika hatua za mwisho kabisa za umaliziaji” alisema Mwali mkuu wa Shule ya Sekondari Mpitimbi
Nae Kaimu mweyekiti wa kamati ya Fedha na wajumbe wake baada ya kukagua na kupitia taarifa, alisema “ kazi ya kamati ni kupitia kukagua na kushauri sehemu zenye mapungufu ili ziweze kufanyiwa kazi, lakini kwako tumejiridhishwa na utendaji wako wa kazi, jengo linaenda vizuri na linaenda kwa wakati. Tumetembelea miradi mingine kama hii yako nikupongeze huu wako unaenda vizuri na unatia moyo.
Aidha kwa niaba ya Uongozi mzima wa Shule, Mkuu wa shule ya Sekondari Mpitimbi alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia pesa kupitia Mradi wa
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa