Kaimu Kamanda wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa wa mkoa wa Ruvuma Owen Jassoni amesema idadi ya wananchi wanaotoa taarifa dhidi ya vitendo vya rushwa imeongezeka toka wastani wa watu 75 hadi 131 kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Machi 2021.
Jassoni ameyasema hayo wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Machi kwa waandishi wa habari katika ukumbi wa ofisi za Taasisi hiyo Manispaa ya Songea hivi karibuni.
Jassoni emesema ongezeko hilo limetokana juhudi za Taasisi hiyo kuwajengea uwezo wananchi kuhusu madhara ya vitendo vya rushwa katika jamii kupitia makongamano,uanzishwaji wa clabu za wapinga rushwa kwenye shule za msingi na sekondari,machapisho na TAKUKURU inayotembea huduma ambayo watumishi wa Taasisi huwafikia wananchi kwenye makazi yao.
Ameongeza kwakusema kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Machi Taasisi imefanikiwa kufanyakazi mbalimbali kama ukaguzi wa miradi ya maendeleo,kutatua changamoto za wananchi dhidi ya kudhulimiwa haki zao,ufuatiliaji wa ruzuku wa fedha za TASAF na kuwafikisha mahakamani waliobainika kuhusika na vitendo vya rushwa.
Jassoni amesema Taasisi hiyo itaendelea na kazi ya kutoa elimu kwa wananchi kwa lengo la kuimarisha uelewa na uwezo wa wananchi kupambana na kupinga vitendo vya rushwa ambavyo vinasababisha ukosefu wa haki na na dhuluma katika jamii.
Jassoni ameitaja mikakati ya utendaji kazi kwa kipindi cha mwezi Aprili hadi Juni ni pamoja na kufuatilia shughuli za miradi ya maendeleo ili thamani fedha ilingane na miradi,itaendelea kutoa elimu ya kupiga vita vitendo vya rushwa na wananchi kuwa tayari kutoa ushahidi pale wanapotakiwa kufanya hivyo sanjari na kuendelea na uchunguzi wa makosa ya rushwa na kuchukua hatua stahiki.
Jassoni ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kuendelea kushirikiana na Taasisi hiyo kukemea, kutoa taarifa za vitendo vya rushwa na kukataa rushwa kwakufanya hivyo mapambano dhidi ya rushwa yatafanikiwa katika jamii.
”sote kwa pamoja tuikatae rushwa”
Imeandaliwa na kuandikwa
Jacquelen Clavery
Afisa Habari
Songeadc
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa