Mkuu wa Wilaya ya Songea Mh Pololeti Mgema ameuagi za uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea kuharakisha ukamilishaji wa ujenzi wa vyumaba sita vya madarasa katika Shule ya Msingi Kivukoni ili wanafunzi waanze kutumia madarasa hayo.
Mh mgema ametoa agizo hilo baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa vyumba hivyo unanyoendelea shuleni hapo hivi karibuni.
Mh Pololeti ameridhishwa na hatua ya ujenzi iliyofikiwa na kuagiza ungozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea kukamilisha shughuli za ukwamishaji milango,madirisha na kupaka rangi kuta na wanafunzi waanze kutumia vyumba kwa kusomea na mazingira mazuri ya kutolea Elimu.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Walmshauri ya Wilaya Songea Bw Saimoni Bulenganija amehahidi kutekeleza majukumu hayo kwa wakati ili wanafunzi wapate mazingira mazuri ya kujifunzia na kufundishia kwa Elimu yenye ubora.
Ujenzi wa vyumba hivyo unafuatia baada ya shule hiyo kupasuliwa na nyufa kubwa mwaka 2014 ambazo zingeweza kuleta madhara kwa wanafunzi endapo wangeendelea kutumia madarasa hayo.
Serikali ilitoa shilingi milioni miamoja na arobaini na moja na nguvu za wananchi zimetumika katika ujenzi wa Madarasa sita yaliyo jengwa katika shule hiyo.
Shule ya Msingi Kivukoni mwaka 2018 imeandikisha wanafunzi wa Awali ishiri na taatu (23) na wanafunzi wa Darasa la kwanza 18 na kufanya idadi ya wanafunzi wote kufikia Zaidi ya 120.
Kwakipindi chote ambacho tatizo limetokea wanafunzi wamekuwa wakitumia jengo mbadala ambalo limejengwa kwa ajili ya kuishi mwalimu
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa