Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajia kuwasili Mkoani Ruvuma siku ya Jumatano Julai 30, 2025, ambapo pamoja na mambo mengine atazindua mradi mkubwa wa Uranium unaolenga kuchochea ukuaji wa Uchumi, ajira na maendeleo ya Viwanda katika Wilaya ya Namtumbo na Ruvuma kwa Ujumla.
Ujuo wa Mhe. Rais. Dkt Samia Suluhu hassan, unatupa fursa nyingine kama Halmashauri ya wilaya ya Songea katika kuendelea kutangaza rasilimali tulizonazo kwani ujio wake huambatana na viongozi mbalimbali ikiwemo viongozi wa Chama na Serikali pamoja na wadau mbalimbli wa maendeleo.
Mgeni njoo, tukwambie usiyoyajua kuhusu Halmashauri ya Wilaya ya Songea. Halmashauri ya Wilaya ya Songea ni miongoni mwa Halmashauri iliyobarikiwa ardhi yenye rutuba ambayo imekua ikizalisha kwa kwingi mazao mbalimbali ya kibiashara ikiwemo zao la Mahindi, Ufuta, Maharage na Kahawa
Halmashauri ya Wilaya ya Songea, ni matajiri wa madini ya Makaa ya Mawe ambayo tangu kugundulika kwake, yamekuwa yakichangia na kuongeza pato la halmashauri.
Halmashauri ya wilaya ya Songea, tumekua tukijivunia maendeleo yaliyofanya na Serikali ya awamu ya sita katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma muhimu kama vile Elimu, Afya,Maji Miundombinu iliyobora, Kilimo na Mahusiano mazuri kati ya Serikali na wananchi.
Songea ipo salama, ujio wako ni fursa kwetu. Karibu Mkoa wa Ruvuma
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa