Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajia kuwasili Mkoa wa Ruvuma mwishoni mwa mwezi huu, ikiwa ni utaraitibu wake wa kuongea na wananchi wake, pia atakua mgeni rasmi kwenye tamasha la tatu la utamaduni la kitaifa litakalofanyika kwenye viwanja vya Majimaji 23.09.2024
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan atazindua tamasha la tatu la utamaduni litakalofanyika Mkoa wa Ruvuma katika viwanja vya maji maji Julai 20-23 mwaka huu. Tamasha hilo limebebwa na kauli mbiu ya “ Utamaduni wetu ni utu wetu, tuuenzi na Kuuendeleza”
Tamasha la utamaduni ni moja ya maagizo ya Rais Samia, akiwa jijin Mwanza mwaka 2021 hivyo kwa utekelezaji wa agizo hilo msimu wa kwanza ulifanyika Dar Es Salaam mwaka 2022, msimu wa pili lilifanyikja mwaka jana Mkoa wa Njombe na huu ni msimu wa tatu ambayo utafanyia Mkoa wa Ruvuma
Matamasha haya yamekua na manufaa mbalimbali kwenye jamii ikiwa ni pamoja na kuenzi utamaduni wetu, kuimalisha utengamano wa taifa, kuitangaza nchi, kutangaza vivutio vya kiutalii na kiutamaduni, fulsa za kiuchumi, kiutamaduni na kijamii, pia kutanua wigo na mitandao ya kibiashara kwa bidhaa zinazozalishwa nchini hususan bidhaa za utamaduni, sanaa na ubunifu
Tamasha hili limeandaliwa na wizara ya Utamaduni, sanaa na michezo ikishirikiana na Taasisi ya maji maji Serebuka na litajumuisha michezo na maonesho mbalimbali kama vile Riadha, Mbio za baiskeli, kushindana kula na kunywa vinywaji na vyakula vya asili, burudai na kazi mbali mbali za sanaa ni miongoni mwa vitu vitakavyonogesha tamasha hilo
Tamasha hili litafungiliwa na Waziri wa utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro, Septemba 20, mwaka huu na kilele chake itakua septemba 23 mwaka huu na mgeni ramsi atakua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo lengo kubwa la tamasha hili la utamaduni pamoja na mambo mengine ni kuenzi utamaduni wetu, na pili kusisitiza umuhimu wa maadili katika Taifa la Tanzania
Aidha baada ya kumalizika kwa tamasha la utamaduni, Mhe. Rais ataanza Ziara katika wilaya sita za Mkoa wa Ruvuma, ambapo Ziara ya kwanza itaanza katika Wilaya ya Songea. Wilaya ya Songea ina Halmashauri tatu na majimbo matatu, Mhe. Rais atatembelea Manispaa ya Songea, Halmashauri ya Wilaya ya Songea na na kisha Madaba.
Kisha Dkt. Samia ataendelea na Ziara yake Wilayani Mbinga, Nyasa, Namtumbo, na Tunduru. Baada ya ziara hizo atahitimisha ziara yake tarehe 28.09.2024 kwa kufanya Matukio mawili, moja Mkutano wa ndani wa UWT Taifa na pili mkutano wa wananchi wote katika viwanja vywa majimaji ambapo ataongea na wanasongea, wanaruvuma na wananchi wote akiwa kwenye uwanja wa Majimaji.,
.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa