Mkuu wa Wilaya ya Songea Mhe Kapenjama Ndile, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mwl. Neema Maghembe wamekutana na Walimu Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari, Maafisa Elimu Kata, Maafisa Tarafa, na Watendaji wa Vijiji na Kata Kwa lengo la kufanya tathmini ya idadi ya wanafunzi waliojiunga na Elimu ya awali, darasa la Kwanza na kidato cha Kwanza.
Pamoja na mambo mengine wamejadilina pia namna ya kuwashawishi wazazi na walezi pamoja na wanafunzi ambao walijiandikisha kwenda shule lakini mpka sasa hawajafika kuripoti Shule, kikao hicho kilifanyika siku ya jana katika ukumbi wa mhe, Jenista mhagama katika shule ya sekondari ya maposeni.
Sambamba na hilo ndile amewaagizaa wakuu wakuu wa shule, maafisa elimu kata, maafisa tarafa na watendaji wa kijiji kuhakikisha kila mwanafunzi mwenye umri wa kwenda shule kwa maana ya watoto wenye umri kuanzia miaka mitano(5) wanakwenda shuleni.
"Nawaagiza watendaji wa kijiji, wakuu wa shule, maafisa elimu kata, na maafisa tarafa wote hakikisheni watoto wote wenye umri wa kwenda shule wanakwenda shuleni kwa sababu serikali imejenga shule nzuri na zenye mazingira mazuri ya kusoma watoto wetu" amesema Kapenjama Ndile
Aidha Mkuu wa Wilaya amewataka watumie mbinu yeyote watakayoona inafaa ili wanafunzi hao wafike shulen Kwa ajili ya kuanza masomo yao.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa