MKUU wa Wilaya ya Songea Mhe. Wilman Kapenjama Ndile amefanya ziara ya ukaguzi wa miradi katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea ameambatana na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Menas Komba, Kaimu Mkurugenzi Lucy Mbolu na timu ya Wataalamu.
Akiwa katika ziara hiyo amekagua ujenzi wa mradi wa BOOST wa madarasa mawili na matundu matatu ya vyoo katika shule ya msingi Kizuka ambapo unatekelezwa kwa fedha kiasi cha shilingi milioni 53.1.
Pia amekagua ujenzi wa mradi wa LANES wa madarasa mawili ya Awali ya mfano wenye dhumuni la kuboresha taalamu kwa madarasa ya Awali katika suala zima la kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK) unaotekelezwa katika shule ya msingi Ngahokora.
Vilevile amekagua ujenzi wa Soko na ghala linalojengwa katika Kijiji cha Matomondo ambapo Halmashauri ilipokea fedha kiasi cha shilingi milioni 198.7 kutoka Serikali Kuu kwaajili ya kutekeleza mradi huu.
Akizungumza katika ukaguzi wa miradi hiyo amewataka mafundi Viongozi kuongeza mafundi wasaidizi ili kuhakikisha kazi inafanyika kwa haraka na kukamilika mapema ndani ya muda uliopangwa.
‘‘Nawasisitiza muongeze kasi katika kutekeleza miradi hii ili iweze kukamilika mapema na sio tu kukamilika mapema pia ikamilike kwa ubora na viwango vinavyotakiwa na kukubalika na Serikali’’, amesema Mhe. Ndile.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa