Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololeti Mgema amepiga marufuku kuendesha mnada eneo la shule ya Msingi Kivukoni katika kijiji cha Nakawale - Mkenda badala yake watumie soko la kimataifa la Nakawale -Mkenda lililojengwa mpakani mwa Nchi ya Tanzania na Msumbiji.
Mgema ametoa kauli hiyo alipofanya ziara ya kikazi ya kutembelea mpaka wa Tanzania na Msumbiji na Soko la Kimataifa la Nakawale – Mkenda kwa lengo la kutoa msisitizo wa usalama wa mpaka huo kufuatia ugojwa wa corona, hivi karibu.
“Serikali imewajengea soko mnataka Serikali iwaletee bidhaa ,Serikali haifanyi biashara” Alisema Mgema.
Amewataka wananchi kuhamishia bidhaa zao katika soko hilo na shughuli zote za mnada, na kupiga marufuku kutumia eneo la shule kufanyia shughuli za mnada ilikuhakikisha soko hilolinafanya kazi iliyokusudiwa .
Wakiongea kwa niaba ya wananchi baadhi ya viongozi wa kijiji hicho wamemshukuru Mkuu wa Wilaya huyo kwa kuwapa ufafanuzi wa matumizi ya soko hilo kwani wao walikuwa hawaelewi kama wanatakiwa kutumia soko hilo,huku wakibaki kuliangalia tu.
Soko la Kimataifa la Mkenda limekamilika kwa asilimia kubwa huku tatizo likiwa niuwekaji wa miundo mbinu ya maji
Aidha wamemwambia Mkuu huyo wa Wilaya kuwa wanakabiliwa na janga la njaa baada ya mazao yao kusombwa na maji kufutia mfua kubwa zilizonyesha kuanzia mwezi Novemba 2019 hadi mwezi machi 2020.
Changamoto nyingine ni ukosefu wa mawasiliano ya simu jambo linalowapa shida kutoa taarifa kwa mamlaka zinahusika pindi wanapopata matatizo
JACQUELEN CLAVERY
AFISA HABARI SONGEA DC
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa