Halmashauri ya wilaya ya songea mkoani Ruvuma imevuka lengo la kuchanja kwa asilimia 120 ya chanjo ya polio ambayo inazui ugonjwa wa kupooza hasa kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano ambao walipangwa kufikiwa.
Kaimu Mganga mkuu wa Halmashauri hiyo Dr.Geofrey Kihaule amesema kupitia zoezi la kampeni maalum ya kuthibiti maambukuzi ya ugonjwa wa polio imefanikiwa kuchanja watoto 26321 kati ya watoto 21896 ambao walilengwa kufikiwa kupitia kampeni hiyo.
Dr Kihaule ametaja sababu ya kuendesha zoezi la kampeni ni kuimarisha kinga hasa kwa watoto wa wadogo chini ya umri wa miaka mitano baada ya Nchi jirani ya Malawi kukumbwa na mlipuko wa ugonjwa wa polio tatizo ambalo linaweza kufika Nchini hasa kwenye mikoa ya mpakani ya Tanzania na Malawi.
Dr. Kihaule ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuwapeleka watoto katika vituo vya kutolea huduma iliwaweze kupata chanjo kwasababu zoezi la utoaji wa chanjo ya polio na chanjo nyingine ni endelevu licha ya siku nne za kampeni kutamatika machi 29/ 2022.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wazazi na walezi wa Kata ya Mhukuru na Peramiho wametoa wito kwa walezi na wazazi ambao wanamwitikio hasi wa kuwachanja watoto wao waondoe fikra potofu na waunge mkono jitihada za serika katika kupambana na tatizo hilo.
“Ukiona watu wanatembea majumbani ujue changamoto tunayo ,tusisubiri hadi moto augue na ugonjwa hauna dawa tuwapeleke watoto wakapate matone”,amesema Salome Awonga mkazi wa kijiji cha Nakawale.
Chanjo ya polio ni chanjo inayotolewa kwa watoto wenye umri wa miaka sifuri hadi miaka mitano ambayo inazuia ugonjwa wa kupooza hasa kwa watoto wadogo wenye umri huo ingawa hata watoto wanaozidi umri huo wanaweza wakakumbwa na tatizo la kuugua polio.
Imeandaliwa na kuandikwa na
Jacquelen Clavery
Afisa Habari
Songea DC.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa