20/03/2024, vyama vinne ambavyo ni ( CCM, UMD, UPDP na DM) viligombea nafasi ya Udiwani katika Uchaguzi mdogo wa udiwani uliofanyika katika kata ya Mbinga Mharule iliyoko katika jimbo la Peramoho, Halmashauri Wilaya ya Songea ambapo Chama cha Mapinduzi CCM kimeibuka Mshindi
Uchaguzi huo ulifanyika jana katika kata ya Mbingamhalule hiyo ili kumpata kiongozi bora atakaye waongoza baada ya aliyekuwa diwani wa kata hiyo kufariki dunia mwezi desemba 2023.
Chama cha Mapinduzi CCM kimeibuka na ushindi kwa kupata kura 4,336 sawa na asilimia 98.7 akifuatiwa na chama cha DM ambaye amepta kura 26 huku UMD akipata kura 23 na UPDP amepata kura 10.
Matokeo hayo yametangazwa na msimamizi wa uchaguzi jimbo la Peramiho bwana, Khashim Sultan Lugome, ambapo amemtangaza ndug, Optatusi Thadei Ndau mgombea kupitia tiketi ya chama cha mapindizi (CCM) kuwa Diwani wa kata ya Mbinga Mharule.
Msimamizi wa Ushaguzi Jimbo la Peramiho Ndg. Khashim Lugomne alisema "Kwa mamlaka niliyopewa namtangaza bwana Optatusi Thadei Ndau mgombea kupitia tiketi ya chama cha mapindizi CCM kuwa Diwani wa kata ya Mbinga Mharule kuanzia leo Tarehe 20/2024"
Wapiga kura waliondikishwa ni 6,120, waliopiga kura ni 4,452,kura halali ni 4,395 na kura zilizokataliwa ni 57
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa