Serikali imetangaza bei elekezi za pembejeo za kupandia na kukuzia kwa msimu wa kilimo wa mwaka 2017/2018 kwa mbolea aina ya dap na urea ilikuondoa mkanganyiko wa bei za mbolea.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya BW SIMONI BULENGANIJA ameyasema hayo hivi karibuni
Bw Bulenganija amesema kwa msimu wa kilimo 2017/2018 mbolea aina ya dap na urea zitauzwa kwa bei ekekezi , urea itauzwa shilingi 41,693na dap itauzwa shilingi 54,272 na pembejeo zipo za kutosha, wakulima wache mashaka juu yaupatikanaji wa pembejo hizo katika Wilaya ya Songea badala yake waongeze bidii ya uzalishji wa mazao.
Bw Bulenganija ametoa rai kwa wakulima kununua pembejeo hizo kwenye vyanzo sahihi ikwemo ghala la serikali la mbolea (TFC) namawakala wanaotambuliwa kisheria ili kuepukana na knunua mbolea zisizo kuwa na ubora hali itakayo pelekea kupata mavuno kidogo au kapata hasara na kushindwa kufikia malengo tarajari.
Halmashauri ya Walaya Songea kwa msimu wa kilimo 2017/2018 inatarjia kuzalisha tani Zaidi ya laki mbili za mahindi sawa na ongezeko la asilimia 10 ukilinganisha na msimu uliopita wa kilimo 2016/2017
Adha amewataka wakulima kuzingatia maelekezo kutoka kwa wataalam wa kilimo kwa matokeo chanya ya mapato yao iliwaweze kujikwamua kiuchumi kwa mtu mmoja mmja, kaya na Taifa kwa ujumla.
Bw Bulengenija amewahamasisha wakulima kulima mazao mbadala ambayo ni kahawa na korosho mazao ambayo yanastawi ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea, kahawa inastawi katika maeneo ya Liganga,Litisha na Mbinga muhalule,na korosho inastawi katika kata ya Lilahi, Muhukuru, Ndongosi,na Maposeni.
Halmashauri ya Wilaya ya Songea ni miongoni mwa Wilaya zinazo tegemewa kwa uzalishaji wa zao la mahindi mkoani Ruvuma hii nikutokana na kuwana udongo wenye rutba na hali ya hewa mchanganyiko pia uhidhi mzuri wa mazingira unaosimamiwa na serikali yaWilaya
IMEANDALIWA NA
JACQUELEN CLAVERY /AFISA HABARI
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa