Afisa Afya wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma John Kapitingana amesema asilimia 87 ya wakazi wa Halmashauri hiyo wanavyoo bora vyenye sifa na uwezo wa kupambana na magonjwa
Kapitinga amezitaja sifa za vyoo bora kuwa ni vile vyenye,milango,sakafu inayoweza kusafishika vizuri, vinavyotunza faragha kwa mtumiaji, pamojana kuthibiti magonjwa ya kuambukiza.
Kapitingana amesisitiza kwamba kupitia ‘kampeni ya nyumba ni choo” Halmashauri kwa kushirikiana na wadau wa afya imefanikiwa kwa asilimia 87 kuhamasisha jamii kujenga vyoo bora ambavyo vinakubalika kwa matumizi ya kibinadamu.
Kampeni ya nyumba ni choo ni elimu inayotolewa kwa wakazi wote nchi ilikuhakikisha wananchi wanajenga na kutumia vyoo bora badala ya kujisaidia ovyo,ovyo na kusababisha kuenea kwa magonjwa ya kuhara ,kipindupindu,kichocho cha tumbo na magonjwa ya milipuko ambayo ni hatari kwa maisha ya binadamu.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Kijiji cha Parangu Patriki Komba amesema wanashukuru wadau wa afya kwa kuanzisha kampeni hiyo ambayo imewasaidia sana kupata uelewa kuhusa umuhimu wa kutumia vyoo bora katika makazi yao.
Amesema katika Kijiji hicho asilimia kubwa ya wakazi wamejitahidi kujenga vyoo bora na maeneo ya kutakasa mikono baada ya kutoka chooni na kutengeneza vichanja kwa ajili ya kuanikia vyombo na usalama wake.
Ametoa wito kwa wadau wa afya kuendelea na kampeni ya nyumba ni choo kwa lengo la kuzifikia kaya zote kwa asilimia miamoja ifikapo julai 2022.
Imeandikwa na
Jacquelen Clavery
Afisa Habari Songea DC
10 /06/2021
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa