Mkuu wa Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Pololet Mgema ametoa maelekezo kwa jeshi la polisi la Wilaya ya Songea kuendelea kufanya uchunguzi wa kuwabaini wezi wanao hujumu miundombinu ya Shirika la umeme kwa kuiba nyaya zamashine za kupozea umeme “tansformer”.
Mgema ametoa maelekezo hayo katika kikao cha kamati ya ushauri cha Wilaya kilicho shirikisha Wilaya ya Songea Manispaa,Madaba na Songea DC kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea hivi karibuni.
“Naomba nitumie kikao hiki,OCD endeleeni kufanya uchunguzi tukimpata yoyote anayehusika tuhakikishe hatarudia tena kufanya tukio hilo”,amesisitiza Mgema.
Mgema ameongeza kwa kusema, jeshi la polisi liendelee kufanya uchunguzi na kuukamata mtandao mzima unajihusisha na hujuma za miundo mbinu ya shirika la umeme Tanzania kwa sababu kitendo hicho kinaisababishia serikali hasara na wananchi kukosa huduma ya umeme.
Kwa upande wake Meneja wa Shirika hilo mkoani Ruvuma Bi.Florence Mwakasege amewarai wananchi kushiriki katika ulinzi wa kulinda miundombinu ya TANESCO kwa kutoa taarifa za wizi au wanapowatilia mashaka watu ambao siyo watumishi wa Shirika hilo wanapokwea kwenye mashine hizo.
Mwakasege amesema hujuma hizo tayari zimelisababishia hasara Shirika kwakutumia fedha ambazo zipo nje na utaratibu kwakukarabati miundombinu ambayo imeibiwa, wananchi kukosa huduma ya umeme kwakuwa nyaya hizo ndizozinazosambaza umeme kupeleka kwa watumiaji matumizi mabaya ya muda kwa watumishi kurudia kazi ambazo zilishafanyika.
Mwakasege ameyataja maeneo ambayo yamekithiri kwa wizi wanyaya hizo kuwa ni Peramiho na Songea Manispaa na nyaya ambazo zinaibiwa ni aina ya kopa ambazo zinaonekana kuwa na soko kubwa ukilinganisha na nyaya aina ya aluminiam.
Baadhi ya wakazi wa Peramiho wamesema kitendo hicho hakikubaliki katika jamii kwani umeme ni kichocheo cha maendeleo,watashiriki katika kulinda mali hizo na kutoa taarifa katika vyombo vya dola watakapotilia shaka kwa mtu yoyote atakaye jaribu kuhujumu miundombinu hiyo.
Imeandaliwa na kuandikwa na
Jacquelen Clavery
Songea DC.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa