Wagombea watakiwa kutumia lugha ya ushawishi wakati wa kampeni.
MSIMAMIZI wa uchaguzi wa jimbo la Peramiho, mkoani Ruvuma, Simon Bulenganija ametoa wito kwa wagombea jimbo hilo kwa nafasi za udiwani na ubunge kuacha kutumia lugha za kuwakatisha taama wapiga kura kwenye zoezi la uchukuaji wa fomu na kampeni
Bulengamija ametoa wito wakati akimkabidhi fomu mgombea ubunge kupitia chama cha mapinduzi Jenista Mhagama katika ofisi za jimbo la uchaguzi la Peramiho baada ya Halmashauri kuu ya Taifa ya chama hicho kumpendekeza kuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM.
Amesema tunapoingia kwenye mikutano ya kampeni za uchuguzi ni vema wagombea wa ubunge na udiwani wakatumia lugha za kuwashawishi wananchi kujitokeza kwenda kupiga kura badala ya kutumia lugha za kuwakatisha tamaa wapiga kura.
Amesema mikutano ya kampeni pamoja na wagombea kuomba kura pia aliwaasa watumie mikutano hiyo kutoa elimu ya mpiga kura kwa wale wenye sifa ya kwenda kupiga kura na kuwachagua viongozi kwani watakuwa wametekeleza demokrasia kwa vitendo.
“Tumesha maliza uchaguzi ” alisema Bulenganija
kauli kama hiyo inakatisha tamaa au inavunja utayari kwa wanachi wenye utayari wa kwenda kupiga kura na Taifa kushindwa kufikia adhima iliyojiwekea
Bulenganija amasisitiza kwa kusema uchaguzi wa mwaka 2020 ni wa huru na haki hivyo kila mgombea na wananchi wakazingatia taratibu, kanuni, na sheria za Tume ya Taifa ya uchaguzi kama inavyo elekeza katika kipindi chote cha mchakato, kupiga kura, kuhesabu na kutangaza matokeo.
Kwa upande wake mgombea ubunge wa jimbo hilo la Peramiho, Jenista Mhagama baada ya kukabidhiwa fomu na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Bulenganija alisema kwa kujinadi kuwa wakati Rais Dk John Magufuli akiwatuma hakuna chama dhidi ya CCM kazi kubwa aliyokuwa mbele yetu ni kuendelea kuwatumikia wananchi wa jimbo la Peramiho katika kuhakikisha maendeleo yanasonga mbele katika sekta ya elimu, afya, maji, miundombinu ya barabara, kilimo na michezo kwa vijana.
Pia amewashukuru wanachama wa chama hicho cha CCM katika jimbo hilo la Peramiho kwa kumpa heshima kupitia kura za maoni hadi kuwa mgombea ubunge kwa kipindi kingine hivyo na kuahidi ushindi wa kimbuka kwa madiwani, wabunge na Rais Dk John Magufuli mkoani Ruvuma
Imeandikwana
Jacquelen Clavery
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa