Baraza la Madiwa Halmashauri ya Wilaya ya Songea liimetaka Wizara ya Habari,Utamaduni na Michezo kuwachukulia hatua waandishi wanao kiuka kanuni,taratiba na sheria za uandishi.
Hayo yamesemwa na baadhi ya Waheshiwa madiwani wakati wakichangia hoja mbalimbali katika mkutano wa baraza maalum la kukanusha habari za upotoshaji,mkutano uliofanyika katika ukumbi wa H/ mashauuri ya Wilaya ya Songea hivi karibuni.
Wameitaka Wizara kufanya hivyo kufuatia baadhi ya waandishi wa habari wa Mkoa wa Ruvuma kuandika habariza za upotoshaji kuhusu Halmashauri ya Wilaya ya Songea bila kufuata taratibu,kanuni,maadili na sheria za uandishi wa habari na kusababisha sintofahamu katika jamii.
Waandihi hao wamedai kwamba Halmshauri ya Wilaya ya Songea imekuwa ikikabiliwa na changamoto za watoto wa shule ambazo ni shikizi kusomea kwenye mabanda ya nyasi na wanakalia kwenye tofari wakati wa kujifunza au kusoma,ukosefu wa walimu,matundu ya vyoo,vyumba vya madarasa na madawati Zahanati kukosa wa watendaji wa afya jambo mambalo halina ukweli wote.
Aidha Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mh Rajabu Hassani Mtiula ametoa wito kwa waandishi wa habari kutumia taaluma yao katika kuchochea maendele katika sekta mbalimbali kama elimu,maji,afya, mazingira,ajenzi wa viwanda vidogovidogo na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambayo ipo na inatekelezwa ndani ya Halmashauri.
Ametaja baadhi ya miradi mikubwa inayotekelezwa ni pamoja na ujenzi wa Kituo cha Afya Muhukuru,ukarabati wa Zahanati katika kata mbalimbali,ujenzi wa mindo mbinu ya barabara,miradi ya maji,na ukarabati wa barabara korofi ili ziweze kupitika muda wote.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa