Viongozi wa Taasisi mbalimbali wamekumbushwa kuheheshimu misingi ya utawala bora pindi wanapotoa huduma kwa waliowapa dhamana kwakufuata taratibu,kanuni na sheria za nchi.
Kauli hiyo imetolewa na Mwezeshaji na Mshauri Mwelekezi Utawala Bora Wakili Lawrence Chuma katika warsha ya Utawala Bora iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma hivi karibuni.
Wakili Chuma amesema Viongozi wa Taasisi mbalimbali wametakiwa kuzingatia sheria,kaninu na taratibu za utawala bora na uwajibikaji katika kuwatumikia wananchi kwalengo la kuwajengea wananchi misingi imara ya kuwabijika na kushiriki kuijenga nchi yao.
“Viongozi mmepata dhana ya kuongoza wananchi hivyo mnapaswa kuzingatia misingi ya utawala bora kwa kutoa taarifa sahihi na kwakutumia lugha nyepesi ambayo itawezesha wananchi kuwa na uelewa”.amesema Wakili Chuma.
Wakili Chuma ameongeza kwa kusema utawala unaozingatia demokrasia,uwajibikaji,ushirikishwaji, maridhiano,haki za binadamu na utawala wa sheria unatoa fursa kwa wananchi kunufaika na rasilimali za nchi kwa pamoja.
Kwa upande mwingine Wakili Chuma amewataka wananchi kuwajibika kikamilifu katika swala zima la kulinda,kusimamia na kutunza rasilimali za nchi ili ziweze kutoa huduma endelevu kwa vizazi vijayo.
Kwa upandewake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika lisilo la kiserikali Millenium Art Group Mnung’a Shaibu Mnung’a ametoawito kwa viongozi kuwajibika kwa wananchi kwa kuwapa taarifa sahihi kwakuitisha mikutano ya hadhara ambayo inatoa fursa kwa wananchi kujadiliana na kuamua kwa pamoja katika kutekeleza mipango yao.
“Tunasisitiza sana viongozi kuitisha mikutano ambayo hailengi tu kuwapa taarifa wananchi kuhuhsu michango na maelekezo mbalimbali “amesema Mnung’a
Amesema wananchi wamekata tamaa ya kwenda kushiriki mikutano ya hadhara kwakujenga dhana ya kwamba kwenye mikutano hiyo agenda ni kupatiwa taarifa za michango mbalimbali na maagizo ya jambo fulani.
Kufuatia hali hiyo Mnun’ga ametoa wito kwa viongozi wa taasisi mbalimbali kuwajibika kutoa elimu kwa wanachi katika kuwashirikisha na kujadili kwa pamoja mipango inayopangwa na serikali na utekelezaji wake ili wananchi nao washiriki kikamilifu.
Millenium Art Group Shirika lisilokuwa la kiserikali limeendesha mafunzo kwa Wakuu wa Idara na Vitengo mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea ambao nao wanatakiwa kuzingatia misingi ya Utawala Bora.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa