Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Wilaya ya Songea Bi Hossana Ngunge, akiambatana na Afisa Nyuki David Kikas, wametembelea kikundi cha Ukombozi TASAF Ngahokola, kukagua mizinga ya nyuki 34 waliowapatia wanufaika hao.
Mizinga hiyo imetokana na fedha za ruzuku ya tasaf walizokuwa wakipata kila baada ya miezi miwili pia na akiba ambayo walikuwa wamejiwekea kwenye kikundi chao.
Lengo la kuwatembelea wanufaika hao ilikua ni kuwayia moyo kwa namna wanavyojishughulisha lakkn pia kuwahamasisha kushiriki Maonesho ya Nane Nane ili waweze kuonesha na kuuza bidhaa zao zinazotokana na nyuki..
Akizungumza Afisa Nyuki wa Halmashauri David Kikas, alisema “ najua mmetoka mbali sana tangu mnamizinga mnne (4) mpaka sasa mnamizinga thelathini na nne (34) ni hatua kubwa sana, mnapaswa kuwashukuru sana TASAF, ila niwakumbushe tu kwamba kupitia nzuki mnawwza pata bidhaa mbalimbali zinazoweza kuwakwamua kimaisha kama vile Asali, Nta ambayo hutengenezea mafuta, mishumaa, Usinde au Chavua, Mkate wa nyuki, Gundi ya Nyuki nk vyote hivi vinaweza kuongeza kipato”
Aidha wanakikundi walishauriwa pia kuwa na mikakati ya mda mrefu katika kutengeneza uhai wa kikundi chao ikiwa ni pamoja na kufungua account, kujisaji na kuanzisha miradi mingine ili kuweza kupanua wigo katika safari yao ya mafanikio.
Hata hivyo kikundi cha Ukombozi Tasaf Ngahokola nimeshukuru sana Serikali na Mbunge na uonhozi wa Halmshauri kwa kuwawwzesha wanakaya masikini lakin pia kitengo cha Nyuki kwa kuwapa ujuzi wa namna yakuendesha mizinga za nyuki.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa