Halmashauri ya Wilaya ya Songea imepokea mbegu za alizeti kwaajili ya kupanda katika mashamba ya shule kutoka kwa Mbuge wa Jimbo la Peramiho Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama.
Zoezi la ugawaji wa mbegu hizo limefanyika katika ukumbi wa Halmashauri Lundusi-Peramiho ambalo limeongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Ndugu Neema Maghembe.
Akizungumza katika zoezi hilo Ndugu Neema ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mhe. Jenista Joakim Mhagama kwa kuweza kuleta Mbegu za alizeti ambazo zinaenda kupandwa katika mashamba ya shule za msingi na sekondari.
“niwaombe maafisa elimu, maafisa elimu kata na walimu wakuu mliopo hapa tuhakikishe mbegu hizi zinaenda kupandwa katika mashamba ya shule, maafisa elimu mkishirikiana na Afisa Kilimo mnapoenda kukagua shughuli za kitaaluma tukakague na mashamba ya shule zitakapopandwa alizeti hizi’’, amesisitiza Ndugu Neema.
Wakizungumza walimu kwa nyakati tofauti wameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan pamoja na Mbunge wa Jimbo la Peramiho kwa kuwaletea Mbegu ambazo zitapandwa katika mashamba ya shule kwakua wanafunzi wanapata chakula cha mchana shuleni alizeti hizo zitaenda kuwasaidia kupata mafuta kwaajili ya kupikia hivyo itawapunguzia wazazi adha ya kununua mafuta.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa