Agizo la kushugulikia malalamiko ya Wananchi, limeletwa katika Baraza la madiwani lilifanyila leo katika Ukumbu wa Halmashauri Lindusi.
Ujumbe huo umewasilishwa leo na Bi. Amina Tendwa kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma.
Akiwasilisha ujumbe huo Bi. Amina amesema
“ Mhe Mwenyekiti, maelekezo mbalimbali yalitolewa kutoka taasisi zetu za juu, Kutoka TAMISEMI, lakini pia Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma.
Sisi kama watumishi wa Umma na Taasisi zote za Umma zinapaswa/tunapaswa kushughulikia malalamiko ya wannchi ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi lakini pia kuimalisha uwajibikaji wa watumishi wa umma katika Taasisi zetu za Kiserikali”
Aidha, Tendwa Ameagiza kuanzishwa kwa Ofisi za malalmiko ikiwa ni sehem ya kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kusimamia na kutekeleza shughuli zote za Kiserikali pamoja na kusikiliza kero za wananchi wetu ambao wammpatia kura Mhe. Rais na viongozi wote wa umma.
Lengo la kushughulika na kero za wananchi, ni kuhakikisha tunapunguza manung’uniko ya wananchi wetu huku tukitimiza yale majukumj yetu ya kimuundo.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa