Kamati ya fedha, Uongozi na Mipango ikiongozwa na Mwenyekiti wake, ambaye pia ni Mwenyekityi wa Halmashauri Mhe. Menans Komba tarehe 30/10/2024 ilianza Ziara ya siku mbili ya ukaguzi wa miradi ya maendelea inayofanyika kwenye kata zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Songea .
Ziara hiyo ilianzia Kata ya Muhukuru, Kijiji cha Nakawale ambapo walikagua ujenzi unaoendelea katika Zahanati, kisha Jenista shule ya Msingi, Zahanati ya Mipeta, Shule ya Msingi Mbiro Shule ya Msingi Uramboni na Zahanati ya Kijiji cha Kizuka.
Akizungumza katika ziara hiyo, Mhe. Komba alisema “ kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango imeendelea na utaratibu wake wa kukagua miradi ya maendeleo, na leo tumepitia maeneo mbalimbali ambayo tulitoa maelekezo kwa wataalam kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kwa kujali fedha ya Serikali.
Leo tumekagua, tunaona mambo yanaenda vizuri, mafundi wapo na vifaa vipo, kazi kubwa imefanyika tumeendelea kuweka msisitizo kazi zote ziishe kwa wakati ili wananchi waendelee kupata huduma ya uhakika.
Tunaendelea kumshkururu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mhe. Jenista Mhagama kwa kweli wanafanya kazi kubwa kuhakikisha wananchi wao wanapata maisha bora.
Msisitizo mkubwa umewekwa kwa mafundi kuhakikisha wanafanya kazi kwa weredi na kiuzalendo, kwani sasa Serikali inaamini uwepo wa mafundi wazawa hivyo kwakua wameaminiwa basi wawatumikie watazanzia kwa moyo.
Aidha Mhe. Komba ametoa wito kwa Mafundi kuendelea kuomba kazi kwenye Mfumo ili Halmashauri iweze kuwapa kazi za ujenzi kwan miundombinu inaendelea kuboreshwa siku hadi siku
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa