Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma imefanikiwa kupunguza ukubwa wa tatizo la ugojwa wa malaria hadi kufikia asilimia15.1 kutokana na mbinu na mikakati ya kupambana na ugonjwa huo ilivyotekelezwa kwa uweledi mkubwa.
Mratibu wa malaria wa Halmashauri hiyo LEAH MHALULE ameitaja mbinu na mikakati waliyoitumia katika kupambana na tatizo hilo kuwa ni kuelimisha jamii kuhusu matumizi bora ya vyandarua kupitia kampeni ya kitanda kwa kitanda, kudhibiti mazalia ya mbu kwa kupulizia dawa ya viuawadudu wanaosababisha vimelea vya malaria,
Mikakati mingine ni pamoja na matumizi ya dawa ya SP kwa akina mama wajawazito sambamba na kuwagawia nyandaru mara wanapoanza kliniki ,ugaawaji wa vyandarua mashuleni na Watoto wenye umri wa miezi tisa .
Mhalule ametoa wito kwa kila kaya kutumia chandarua wakati wa kulala na kuto puuza matuzi ya chandarua kwa sababu chandaru ni kinga namba moja katika kupambana na maambukizi ya vimelea vya malaria na matumizi ya dawa ya SP kwa wajawazito.
“Viongozi wa Serikali na wadau wa kupambana na malaria wekeni agenda ya Elimu ya kupambana na malaria kuwa ya kudumu katika vikao kama UKIMWI nia ikiwa kupambana na kutokomeza ugonjwa wa malaria, na malaria kuwa historia katika jamii”,amesema Mhalule.
Mhalule amesema kwa kipindi cha mwaka 2017,2018, ukubwa wa tatizo la malaria ulikuwa wastani wa asilimia 58 ukilinganisha na mwaka 2020 hadi kufikia mwezi Septemba ukubwa wa tatizo la ugonjwa malaria ulishuka mpaka kufikia asilimia 15.1
Kwaupande wake Afisa Afya wa Wilaya hiyo JOHN KAPITINGANA amesema kuelekea msimu wa mvua Wilaya imepokea dawa za viuawadudu lita 640 kutoka wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na wototo kwa ajili ya kupuliza kwenye mazalia ya mbu katika vijiji 10 ambavyo vina idadi kubwa ya maabukizi ya vimelea vya malaria ukilinganisha na vijiji vingine.
Amewashukuru wananchi wamekuwa na mwitikio chanya kwa kutoa ushirikiano katika kufanikisha kampeni na upuliziaji wa dawa na kuiomba Serikali kuongeza ujazo wa dawa za viuawadudu kwa sababu iliyopokelewa haikidhi mahitaji ya kuvifikia Vijiji vyote 56 vya Wilaya hiyo.
Kapitingana amevitaja Vijiji vilivyopata kipaumbele kufuatia ukubwa wa tatizo kuwa ni Peramiho A na B, Mpitimbi A na B, Litowa Parangu,Muhukuru Lilahi na Barabarani,Namatuhi na Nakahuga.
Ametoa wito kwa wananchi kufika katika vituo vya kutolea huduma za Afya kwa maana ya Zahanati Vituo vya Afya na Hosiptali kwa uchunguzi na tiba mara wanapo hisi homa badala ya kujitibia majumbani pasipo kufanyiwa uchunguzi.
Ugonjwa wa malaria bado ni tisho kwa afya ya binadamu na Mkoa wa Ruvuma ni wa 5 kitaifa kwa ukubwa wa tatizo la malaria kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2017 zilizotolewa na shirika la Takwimu (NBS) Tanzania.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa