Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wa Mkoa wa Ruvuma Ndugu Oddo Mwisho ametoa wito kwa Viongozi wa Wilaya ya Songea kutoa mikopo na fursa za ajira kwa vikundi vya vijana.
Mwisho ametoa rai hiyo alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua mradi wa shule ya sekondari ya Jenista Mhagama inayojengwa katika Kata ya Parangu wilayani Songea mkoani Ruvuma.
Mwenyekiti huyo akiwa ameongozana na wajumbe wa Kamati na Siasa ya Mkoa wa Ruvuma,katika mradi huo alikagua majengo ya madarasa,majengo ya hosteli,maabara na jengo la utawala ambapo serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni moja ili kutekeleza mradi huo.
”Wakopesheni vijana mikopo wapate fedha ,wafanyekazi za kufyatua tofari ili waweze kurejesha mikopo yao kwa wakati”,amesema Mwisho.
Amesema fursa za mikopo na ajira ambazo vijana watazipata zitawasaidia kujikwamua kiuchumi licha ya kurejesha mikopo yao kwa wakati.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Neema Maghembe amesema katika bajeti ya mwaka huu, Ofisi yake imetenga kiasi cha shilingi milioni 129 kwa ajili ya kuwakopesha vijana,wanawake na wenye ulemavu .
Maghembe ametoa rai kwa makundi hayo kuzingatia vigezo na taratibu zilizoainishwa na Serikali vya kuomba na kukopeshwa fedha hizo pasipo na upendeleo wowote.
Aidha katika ukaguzi huo wajumbe wa kamati hiyo wamesifu na kupongeza jitihada kubwa zinazofanywa na viongozi na wataalam katika kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa miradi hiyo ambayo imejengwa kwa ubora na miongozo iliyoelekezwa na Serikali.
Kamati ya Siasa ya mkoa imetembelea na kugagua miradi minne ya maendeleo ambayo n iujenzi wa Bweni la wasichana na Maabara katika Shule ya Sekondari Matimira, ujenzi wa Shule ya Sekondari Jenista Mhagama inayoendelea kujengwa Kata ta Parangu,matundu ya vyoo na madarasa mawili katika Shule za Sekondari Nalima iliyopo Kata ya Litisha na Mbingamharule.
Imeandaliwa na kuandikwa na
Jacquelen Clavery
Afisa Habari
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa