Mwenyekiti wa Bodi ya Afya Ngd. Pirmin Mbilinyi akiongozana na msafara wa wajumbe 12 wa Bodi ya Afya kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa huduma zinazotolewa na changamoto zinazojitokeza katika vituo vya kutolea huduma za Afya.Ziara imefanyika katika maeneo mbalimbali ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Wajumbe waliweza kutembelea Zahanati 5, vituo vya Afya 2,kituo 1 kinachosimamiwa na Parokia, Hospitali ya Wilaya, ambazo ni: Zahanati ya Maposeni, Zahanati ya Parangu, Zahanati ya Peramiho B, Zahanati ya Matomondo, Zahanati ya Lipokela, Kituo cha Afya cha Liganga, Kituo cha Afya Magagura na Hospitali ya Halmashauri Mpitimbi.
Akizungumza kwa niaba ya wajumbe mwenyekiti wa bodi alisema “Lengo kuu la kutembelea vituo vya kutolea huduma za Afya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea ilikuwa ni kujionea vituo vya kutolea huduma ya Afya na kuona aina mbalimbali za huduma za Afya kwa kuzingatia miongozo inayotolewa na Wizara ya Afya Sambamba na hilo Bodi ilikusudia kubaini changamoto ambazo zinaikabaili sekta hiyo ya Afya ili iweze kuishauri Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea”
Kazi mbali mbali zilizofanywa na wajumbe ni kama ifuatavyo, moja maswali kwa wataalam wa Afya kuhusu huduma za Afya wanazotoa kwa wananchi na kupata maelezo na ufafanuzi. Ukaguzi wa miundombinu ya vituo vya kutolea huduma za Afya Ukaguzi wa vifaa tiba na huduma za Afya zinazotolewa, Ushauri na hamasa kwa wataalam hao kuhusu maadili mema ya Utumishi wa Umma kwa jamii, Ushauri wa jumla kuhusu namna bora ya utoaji huduma bora za Afya kwa wanajamii.
Aidha wajumbe walishauliwa kutoa elimu ya usafi, kuhakikisha wataalam wanatoa msukumo katika kutatua changamoto zinazopatikana ili huduma bora iweze kupatikana katika jamii. Hata hivyo Mwenyekitiki wa Bodi baada ya kupokea changamoto ambazo wauguzi wamekuwa wakipitia, alisisitiza Uvumilivu na Uadilifu wakati changamoto zao zinaenda kufanyia kazi
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa