Baraza la madiwani.
Mwenyeki wa halmashauri ya Wilaya ya Songea mh Rajabu Mtiula ameagiza wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2018 wawe wamefika katika shule walizo pangiwa ndani ya Siku saba
Ametoa agizo hilo kufuatia taarifa ya kamati ya kudumu ya Elimu,Afya na Maji iliyowasilishwa na mwenyekiti wa kamati hiyo Mh Mendrad Soko kunawanafunzi walio chaguliwa kuanza kidato cha kwanza bado hawajafika katika shule walizo pangiwa katika kikao cha wazi cha baraza la madiwani kilicho fanyika katika ukumbi wa lhalmashauri hiyo hivi karibuni.
Mh Mtiula amewataka watendaji wa kata na vijiji kuhakikisha wazazi au walezi wanatekeleza agizo hilo na yeyote atakaye kaidi agizo hilo achukuliwe hatua za kisheria pamoja na kufikishwa mahakamani.
Halmashauri ya wilaya ya songea inawanafunzi 161 ambao bado hawajafika katika shule walizo pangiwa.
Jambo ambalo linalorudisha nyuma jitihada za Mh Raisi wa awamu ya tano Dkt John Pombe Magufuli zakutaka watoto wote wanapata Elimu bure kuanzia ELimu ya msingi na sekondari
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa