Halmashauri ya Wilaya ya Songea imetekeleza mpango wa kuthibti kuenea kwa ugonjwa wa malaria kwa kupuliza dawa ya viuavidudu katika maeneo yaliyo tambuliwa kuwa na mazalia ya kudumu ya mbu kufuatia agizo la Mh Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania JOHN POMBE MAGUFULI
Hayo yamesemwa na mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Songea Bw SAIMONI BULENGANIJA wakati wa kampeni ya uhamasishaji wa kuthibiti kuenea kwa ugonjwa wa malaria uliofanyika katika kijiji cha Mpitimbi.
BW BULENGANIJA Amesema Halmashauri imeanza kutekeleza mpango huo kufuatia agizo la Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh JOHN POMBE MAGUFULI agizo alilo litoa wezi Juni .22. 2017 Na kuzitaka Halmashauri zote,Manispaa zote na Majiji kwenda kuchukua dawa hizo na kuzipuliizia kwenye makazi ya watu. Alipokuwa akifungua kiwanda chaViuatilivu Kibaha Mkoani Pwani
Bw Bulenganija ameyataja maeneo yaliyobainika kuwa na mazalia ya kudumu ya mbu na kupuliziwa dawa kuwa ni Nakawale, Nakahuga , Matimira, Magagura, Mbinga muhalule,na Muhukuru.
Sambamba na upulizwaji wa dawa ya viua vidudu Elimu ya afya ya kujikinga dhidi ya ugonjwa wa maralia ime endelea kutolewa kwa wananchi hasa wa vijiji vya Peramiho,Mpandangindo,na Mpitimbi ikishirikisha Maafisa afya, Wahudumu wa afya na watendaji wakata zote za Halmashauri ya Wilaya ya Songea
Bw Bulenganija amesema sambamba na zoezi la upuliziaji dawa nivema wananchi wachukue tahadhari kwa kufanya usafi wa mazingira, kuuwa mazalia ya mbu nakutumia chandarua kwa usahihi wakati wa kulala .Ugonjwa wa malaria ni miongo mwa magonjwa yanayo hatarisha uhai wa binadamu kwakusababisha vifo na umasikini wa kipato kwawananchi
KWAPAMOJA TUNAWEZA SHINDA ; AFRIKA BILA MALARIA INAWEZEKANA
IMEANDALIWA NA;AFISA HABARI
HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA
JACQUELEN CLAVERY
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa