Waziri mkuu wa Jamuhuri ya muungano Tanzania MH KASIMU KASIMU MAJALIWA ameagiza uongozi wa Halmashauri ya Wilayaya Songea kuhamasisha kilimo cha mazao ya biashara ambayo serikari
imeyawekea mkakati kwalengo la kuongeza mapato ya serikali na kuinua uchumi wa wananchi wake.
MH WAZIRIMKUU MAJALIWA amasema hayo wakati akizungumza na watumishi na WAH madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea katika ukumbi wa Halmashauri hivi karibuni katika ziara yake ya kikazi
MH WAZIRI MKUU MAJALIWA ameuagiza uongozi wa Halmashauri kutilia mkazo na kuhamsisha kilimo cha mazao ya biashara amayo ni kahawa na tumbaku ambayo yanastawi katika wilaya ya Songea kwalengo kuongeza mapato ya serikali na wananchi wake.
Amesema kuanzia hatua ya awali ya maandalizi ya shamba mkulima asiachwe pekeyake wataalamu wa kilimo washirikiane kikamilifu katika kuandaa shamba hadi mavuno.
Kufuatia hali hiyo amewataka maofisa ugani kukaa vijijni kutatua changamoto za wakulima badala ya wakulima kuwafuata wa taalamu makao makuu ya wilaya na suala la kilimo ni suala nyeti lazima lisimamiwe ipasavyona kwa umakini mkubwa
Amewataka watumishi kubadilika wanapotekeleza majukumu yao ya kazi waache kukaaa ofisini waende vijijini wakawatumikie wananchi nakubaini changamoto zao kwakuwa huo ndio mpango kazi wa serikali za mitaa pia waache mambo yanapoteza muda katika kufanya kazi
Aidha ametoa wito kwa madiwani kushirikiana na wataalam katika kusimamiaujenzi wa miradi na kuhakikisha inajengwa kwa kiwango kinachotakiwa iliweze kudumu kwa muda mrefu nainakamilika kwa wakati
Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma ina hali ya hewa nzuri na udongo unaofaa kwa kilimo na fursa za uwekezaji
IMEANDALIWA NA JACQUELEN CLAVERY
AFISA HABARI HALMASHAURI SONGEA
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa