KAMATI ya fedha inayoongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mheshimiwa Menas Komba imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi inayotekelezwa Songea Vijijini.
Ziara hiyo ya ukaguzi imefanyika kuanzia tarehe 03 hadi tarehe 04 Mei 2023.
Ukaguzi huo umefanyika katika Kijiji cha Magima ambapo kuna ukamilishaji wa Zahanati iliyoanza kujengwa kwa nguvu za wananchi, Mfuko wa Jimbo ulichangia fedha kiasi ch shilingi 530,000 pia fedha kiasi cha shilingi Milioni 50 zilipokelewa kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo.
Pia ukaguzi huo umefanyika katika Kata ya Mbinga Mhalule Kijiji cha Matomondo ambapo kuna utekelezaji wa ujenzi wa soko la kimkakati na ghala ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Songea ilipokea fedha kiasi cha shilingi Milioni 198,700,650 kutoka Serikali kuu kwaa ajili ya kutekeleza mradi huo.
Vilevile ukaguzi huo umefanyika katika Kata ya Matimira Kijiji cha Matimira B ambapo kuna ujenzi wa Zahanati ambayo ilianzishwa kujengwa kwa nguvu za wananchi, pia Halmashauri ya Wilaya ya Songea Imepeleka fedha kiasi cha shilingi Milioni 50 kutoka mapato ya ndani kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo.
Kwa nyakati tofauti wakizungumza Waheshimiwa Madiwani wa kamati ya fedha wamewasisitiza Viongozi wa Kata na Kijiji kusimamia miradi hiyo kwa umakini ili kuhakikisha inakamilika kwa viwango na kuendana na thamani ya fedha.
Vilevile wananchi wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama kwa kuendelea kuleta fedha ambazo zinatatua changamoto mbalimbali.
Pia wameshukuru Viongozi wa Chama, Baraza La Madiwani na Uongozi wa Halmashauri kwa usimamizi mzuri wa miradi hiyo.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa