Mbunge wa Jimbo la Peramiho na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Joakim Mhagama ametoa wito kwa wazazi kupeleka watoto shule.
Wito huo ameutoa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Nakawale.
“Serikali yetu ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuboresha miundombinu katika sekta ya elimu hivyo wazazi jitahidini kuwaandikisha watoto katika elimu ya Awali na Msingi vilevile Sekondari”, amesisitiza Mhe. Jenista.
Sambamba na hilo Mheshimiwa Waziri amewasisitiza Wananchi wasiuze mahindi yote hivyo amewataka kuhifadhi mahindi hayo kwa ajili ya chakula.
Aidha, Mheshimiwa Jenista ametoa rai kwa Wananchi kuendelea kutunza mazingira kwa kupanda miti katika maeneo yao na maeneo yote yaliyo karibu na vyanzo vya maji.
Ameongeza kuwa Wananchi wote ambao walikopeshwa mikopo ya asilimia 10 kutoka Halmashauri wafanye marejesho ndani ya muda uliopangwa ili mikopo hiyo iweze kukopeshwa kwa watu wengine.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa