KIKAO cha baraza la Madiwani cha robo ya tatu Halmashauri ya Wilaya ya Songea kimefanyika katika ukumbi wa mikutano Lundusi-Peramiho Mei 13 2023 . Kikao hicho kimeudhuriwa na Katibu Tawala, Waheshimiwa Madiwani, Wakuu wa Idara na Vitengo, Viongozi kutoka taasisi mbalimbali kama TRA, TAKUKURU, kamati ya Usalama ya Wilaya Pamoja na Watendaji wa Kata.
Lengo la kikao hicho ni kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo yahusuyo Halmashauri ya Wilaya ya Songea katika Nyanja mbalimbali, vilevile ni Pamoja na kupokea taarifa za utekelezaji wa kamati mbalimbali kwa kipindi cha robo ya tatu ya Januari-Machi 2023.
Akizungumza Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Simon Kapinga Kwa niaba ya Madiwani alitumia nafasi hiyo kuipongeza na kuishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Daktari Samia Suluhu Hassan na Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama Kwa kuendelea kutoa fedha nyingi za miradi jambo ambalo linaleta faraja Kwa wananchi kwa kusogezewa huduma muhimu karibu na maeneo yao.
Aidha, katika baraza hilo Makamu Mwenyekiti alitoa rai kwa Afisa Ushirika na wataalamu kuhakikisha wanafuatilia kwa umakini Vyama vya Ushirika ambavyo wananchi wanavitumia kuuzia mazao yao katika mfumo wa stakabadhi ghalani kuhakikisha havina madeni ili wananchi waweze kuuza mazao yao na kupata fedha zao moja kwa moja.
Pia Katika kikao cha baraza la Madiwani cha robo ya tatu ya Januari-Machi 2023 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Ndugu Neema Maghembe aliishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan na Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mheshimiwa Jenista Joakim Mhagama kwa kutoa fedha nyingi za miradi ya maendeleo.
Vilevile amewashukuru Waheshimiwa Madiwani, Viongozi wa Chama, Timu ya Wataalamu Pamoja na Watendaji wa Kata na Vijiji kwa kuendelea kushirikiana, pia amewasisitiza kuendeleza ushirikiano huo katika kutekeleza na kusimamia shughuli za maendeleo ili Halmashauri isonge mbele Zaidi.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa