Mkuu wa Wilaya ya Songea Wilmani Kapenjama Ndile amewataka wanawake wa Halmashuri ya Wilaya ya Songea kishikamana na kufuata taratibu za vikundi vyao ili waweze kukua kiuchumi. Ameyasema hayo wakati akizungumza na wanawake wa Halmashuri ya Wilaya ya Songea kwenye uzinduzi wa jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi ambapo Kiwilaya umefanyika tarehe 16 octoba 2023 katika ukumbi wa Mama Mkuwa Namihoro Peramiho.
Pia Mkuu wa Wilaya ya Songea amewashauri wanawake wengine ambao walinufaika na mikopo isiyokuwa na riba ambayo ilitolewa kupitia Halmashuri ya Wilaya ya Songea kuweza kurejesha mikopo hiyo ili na wengine waweze kunufaika. Amesema.
"Zamani wanawake walichukuliwa kama viumbe dhaifu sana hata walipokuwa wakianzisha vikundi vyao ilikuwa ni rahisi kuvunjika kwasababu ushirikiano ulikuwa mdogo kwahiyo vikundi vyao vilivumjika kwasababu vilikosa nguvu, lakini kwa sasa mambo yamebadilika wanawake mmetawala kila upande na mkiaminiwa mnaweza sasa kupitia jukwaa hili kwenye vikundi vyenu mnatakiwa kujenga misingi imara ili kufanya kikundi chenu kusonga mbele hususani kwenye masuala ya muda, watu wengi Wanafeli mambo yao kwasababu ya kutozingatia muda kwahiyo niwaombe wanawake mliopo hapa na wengine huko kuzingatia taratibu zote mnazojiwekea kwenye kikundi ".
"Pia katika risala iliyosomwa hapa nimesikia kuna baadhi ya vikundi havijarejesha marejesho yao jambo ambalo linakwamisha maendeleo ya wengine kwasababu Raisi wetu anania njema na wananchi wake ndiomaana alitoa fungu kwaajili ya kuwezesha vile vikundi sasa kama kunawengine hawajarejesha tunamvunja moyo Raisi wetu kwahiyo nichukue fursa hii kuwaomba wote ambao hawajarejesha mikopo warejeshe ili na wengine wanufaike" alisema Kapenjama Ndile Mkuu wa Wilaya ya Songea.
Nae Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya Songea ambaye pia ni Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashuri ya Wilaya ya Songea Bi. Zawadi Nyoni ametoa Shukrani zake kwa Mkuu wa Wilaya ya Songea kwa kuitikia wito wa kuja kuwazindulia jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi ambapo pia amewaomba wanawake waliohudhuria kwenye jukwaa hilo kuwa mabalozi kwa wanawake wengine kwa kuyatendea kazi yale yote yaliyosemwa pale. Ambapo uzinduzi huo umeenda na Kaulimbiu isemayo WEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI ILI KUJENGA TANZANIA YA VIWANDA
Pia pamoja na mambo mengine wanawake wa Songea wamepata mafanikio kadha wa kadha kutokana na shughuli zao za kiuchumi kupitia vikundi vya wanawake pia wanafursa ya kuwezeshwa mikopo kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ambapo hutenga asilimia 4 kwaajili ya utoaji wa mikopo kwa vikundi vya wanawake, ambapo kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 jumla ya kiasi cha shilingi 86,103,944.00 ilikopeshwa kwa vikundi 14 vya wanawake na mwaka 2022/2023 jumla ya shilingi 66,241,815.11 zilikopeshwa kwa vikundi 10 vya wanawake. Hivyo jumla ya shilingi 152,345,759.11 imekopeshwa kwa vikundi 24 vya wanawake kwa kipindi cha miaka miwili ya fedha.
Mikopo hiyo Haina riba ambapo imesaidia sana kuinua mafanikio ya wanawake baadhi ya mafanikio hayo ni pamoja na vikundi vya wanawake kujiimariaha kimiradi kama vile ufugaji wa kuku, kilimo cha mbogamboga, uoteshaji wa uyoga, kilimo cha mahindi, ufugaji wa nyuki na viwanda vidogovidogo vinavyozalisha bidhaa mbalimbali kama vile mikate.
Pamoja na mafanikio wanayoyapata wanawake hao wajasiliamali wameeleza changamoto wanazokutananazo ikiwa ni pamoja na kufanyiwa vitendo vya ukatili, kukosa mitaji mikubwa ya kuweza kuendeleza shughuli zao za kiuchumi, kukosa haki ya kumiliki ardhi hususani wanawake wanaoishi vijijini, pia wanakosa masoko ya bidhaa wanazozizarisha, kukosa haki ya kumiliki uchumi na kipato cha Kaya, pia kutelelezwa na watoto.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa