Wenyeviti wa mitaa wateule na wajumbe kutoka katika kata 16 za Halmashauri ya Wilaya ya Songea wameapishwa leo Novemba 28, 2024 katika Ukumbi wa Jenista Mhagama uliopo Maposeni Sekondari.
Akizungumza katika hafla ya kuwaapisha viongozi hao, Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Peramiho ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri Songea, Bi Elizabeth Mathias Gumbo amewatakia heri viongozi hao katika kazi zao na pia kawataka wakatimize kazi zao kwa uadilifu na kwa uaminifu mkubwa.
Bi Elizabeth Gumbo, Amewataka viongozi wateule kuhakikisha wanaenda kuwa msaada kwa kumsaidia Mhe. Rais kutatua kero kwa Wananchi, na sio kwenda kuongeza Kero, wahakikishe wanashirikiana na wataalam kutatua migogoro inayoibuka kwani ni nafasi yao sasa kuhakikisha wananchi wanapata msaada
Aidha Amewataka viongozi hao waende kutimiza ahadi zao walizowaahidi wananchi kwenye kipindi cha kampeni.
“Ahadi mlizotoa kwa wananchi ndio zimepelekea mmechaguliwa, hivyo hakikishen mnaenda kuzimiza ahadi hizo ili kuweza kukisaidia Chama na Serikali”
Hakimu Mkazi wa mahakama ya mwanzo, Maposeni Mhe. Maryam Burugi wakati akiwaaapisha Viongozi wateule katika ukumbi huo wa Jenista Mhagama uliopo Shule ya Sekondari Maposeni Viongozi hao waliochaguliwa na wananchi katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Novemba 27, 2024 ameasihi wateule hao kutii kiapo hicho kwani kwenye kinyume na kiapo unakua umevunja sharia na utahukumiwa
Uapisho huo ni hatua rasmi unaoonesha sasa ninyi ni viongozi na mnaanza kutekeleza majukumu yenu kwa mujibu wa sharia hivyo mnapaswa kuheshimu na kutii kiapo hiki,
Aidha amewashauri kuhakikisha wanadumisha maadili, uwazi, na uwajibikaji katika utendaji kazi wao ili kufanikisha maendeleo endelevu ndani ya Halmashauri ya ya Wilaya ya Songea Hakimu
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa