Wawezeshaji kutoka Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, jana 08/01/2024 wamefika Halmashauri ya Wilaya ya Songea ili kuwajengea uwezo Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
Dr.Elisei Lubuva, moja ya Wadhiri kutoka. Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo amesema “ lengo la kuwajengea uwezo wenyeviti hao ni kuhakikisha wanatambua kanuni na sheria za kazi zao na maelekezo kuhusu muundo wao wa majukumu ili kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa weredi
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea pamoja na Mkurugenz Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea iwameongoza mafunzo kwa Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji kwa lengo la kuwajengea uwezo.
mafunzo hayo yaliohudhuliwa na Wenyeviti kutoka vijiji 56 vilivyopo Halmashauri ya Songea pamoja na vitongiji 450, yalifanyika katika ukumbi wa Maposeni na Mpitimbi.
Akizungumza katika Mafunzo hayo Mhe. Menans Komba ambaye ndiye Mwenyekiti wa Halmashauri alisema “ Ili uwe kiongozi bora, lazima ujue majukum yako, na mipaka yako. Na sisi kwa kuzingatia hilo, tunafanya mafunzo haya ili kuhakikisha mnapata uelewa ili mkafanye majukumu yenu kwa kufuata taratibu na miongozo”
Mhe. Komba amesisitiza katika usimamizi wa Rasilimali na utatuzi wa migogoro.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halnashauri Bi. Elizabeth Gumbo amewataka viongozi hao kuwa makini katika ukusanyaji wa Mapato.
Vijiji vinamapato, na baadhi ya viongozi wamekua wakitumia Fedha hizo bila kufata utaratibu,
Niwaombe sana mafunzo haya yakawasaidie kupata uelewa na yawe chachu ya maendeleo katika maeneo mnayosimamia”
Aidha Viongozi hao walishukuru kwa mafunzo hayo kwani yatawasaidia sana katika kutimiza majukumu yao
“ Nishukuru sana Utawala wa Awamu ya Sita kwa kuona tunapaswa kupata mafunzo haya ili kuweza kumsaidia Dkt. Samia Suluhu Hassan, niwapongeze uongozi wa Halmashauri kwa kusimamia jambo hili niahidi sisi kama viongozi tutafanyia kazi yale yote tuliyofundishwa.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa