Waziri wa mifugo na uvuvi Luhaga mpina ameagiza mnada wa Upili uliopo katika eneo la la Mtyangimbole wilayani Songea mkoani Ruvuma likabidhiwe Halmashuri ya Madaba.
Waziri Mpina ametoa agizo hilo baada ya kutembelea na kukagua mnada huo katika ziara ya kikazi wilayani Songea.
Mpina ameziagiza Halmashauri za songea na madaba kukabidhiana soko hilo haraka ili serikali iweze kuendelea na taratibu za ukarabati wa soko hilo ili liweze kuingiza mapato ya serikali.
“Naagiza makabidhiano yafanyike haraka ili Halmaashauri inayo husika na uendeshaji wa soko hilo ifanye utekelezaji wake na maduhuli ya serikali yakusanywe kulingana na sheria za Nchi’’,amesisitiza Mpina.
Aidha ametaka ukarabati ufanyike mara moja na kuajiri mlinzi wa muda atakayehusika na kulinda usalama wa eneo hilo na kuhakikisha mnada unafanyika ndani na siyo nje ya jengo kama ilivyo sasa hivi sasa ambapo mnada huo umekuwa uikiingizia kiasi cha wastani wa shilingi milioni 18 kwa mwaka.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Pololet Mgema amesema soko la mnada la Mtyangimbole lilikuwa likimilikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Songea kabla ya Halmashauri hizo kugawanywa mwaka 2014 na uendeshaji wake kufanywa na Halmashauri ya wilaya ya Songea huku maduhuli yakikusanywa na Halmashuri ya Madaba.
Wadau wameishukuru serikali kwa maamuzi hayo na ukarabati ambao utaboresha mazingira ya kutolea huduma na kuimarisha biashara kwa sababu mazingira bora na mazuri humvutia mteja kuja kupata huduma bora.
Imeandikwa na Jacquelen Clavery
Afisa Habari Songea DC
Januari 7,2020
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa