Waziri Mkuu awataka watendaji kutoa elimu ya uwekezaji
Waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Majaliwa Kassim Majaliwa ameagiza watendaji wa serikali kutoa elimu ya uwekezaji kwa wananchi ili waweze kutambua umuhimu wa uwekezaji.
Ametoa agizo hilo wakati anazindua kongamano la uwekezaji na viwanda lililo fanyika kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea.
“Elimu ya uwekezaji itawawezesha wananchi kuingia kwenye uchumi wa viwanda na kuliletea taifa fedha ambazo sitasaidia katika ujenzi wa miradi ya kimkakati’’,amesisitiza.
Amesema mkoa wa Ruvuma ni mkoa pekee wenye fursa nyingi za uwekezaji hivyo watendaji wajenge mazingira mazuri ya kuwashawishi na kuwavutia wawekezaji waweze kuwekeza katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amesema mkoa baada ya kuzindua kongamano la uwekezaji na viwanda unatarajia kutumia malighafi zilizopo ndani ya mkoa zitumike na kuongeza thamani kama vile misitu na madini .
Aidha amesema Mkoa wa Ruvuma una hekta milioni nne ambazo zimetengwa kwa ajili ya uwekezaji lakini zinazotumika ni hekta Zaidi ya lake nane tu huku hekta Zaidi ya laki tatu hazijatumika mpaka sasa.
Aidha aliendelea kusema kuwa hali ya upatikanaji wa huduma muhimu kama barabara, maji, umeme, huduma za afya ipo vizuri katika Mkoa wa Ruvuma.
Naibu waziri wa wizzara ya viwanada na biashara eng stella manyanya alisema uwekezaji kati amkoa wa Ruvuma unachagiza kauli mbiu ya serikali ya uchumi wa viwanda ifikapao 2025.
Mpaka sasa Mkoa wa Ruvuma una jumla ya viwanda 3852 kati ya hivyo viwanda Zaidi ya 3000 ni vidogo sana na viwanda vikubwa ni vinne.
Jacquelen Clavery
Afisa Habari songeadc
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa