WAZEE wa adhimisha siku yao wakiomba Sera ya wazee kutungiwa sheria
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Songea Martini Mtani amesema hayo katika maadhimisho ya siku ya wazee duniani yaliyofanyika katika uwanja wa tamasha mji mdogo Peramiho.
Mtani amesema wazee wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea wameadhimisha siku yao huku wakiomba Serikali kuwasaidia SERA ya wazee kutungiwa sheria ambayo itawasaidia kutetea na kusimamia haki na maslahi ya wazee nchini.
Amezita baadhi ya changamoto zinazo wakabili wazee ni pamoja na umaskini,maradhi ya mara kwa mara,ukatili wa kuuwawa , kuelemewa na mzigo mkubwa wa wategemezi, mmomonyokoko wa maadili katika jamii na kutoshirikishwa kwenye maamuzi mbalimbali yanayohusu maendeleo ya nchi.
Katibu wa Baraza la wazee wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Phillip Katyale ametoa wito kwa jamii kuwatunza wazee na kuacha vitendo vya ukatili dhidi ya wazee kama vile kuwauwa kwa Imani za kishirikina na kuwapa na fasi za maamuzi kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa.
Amesema katika kubaini na kutatua changamoto za wazee ,wazee wameunda mabaraza ya wazee kuanzia ngazi ya Kijiji hadi Halmashauri lengo likiwa kupata fursa ya kubainisha changamoto zao na kubadilishana mawazo kupitia vikao vyao.
Kwa upande wake Mganga mkuu wa Wiliya ya Songea amesema halmashauri imetenga bajeti ya kutengeneza vitambulisho vya bima ya afya ambavyo vitawasaidia kupata huduma ya matibabu bure.
“Familia na jamii tuwajibike kuwatunza wazee,” ni kauli mbiu ya siku ya wazee duniani kwa mwaka 2020
Halmashauri ya wilaya ya songea inawazee wapatao 10543 ambao kati yao 4982 ni wanaume na wanawake 5561 ambao jamii inatakiwa kutekeleza wajibu wao kwakutoa kipaumbele kwa wazee kwakutambua haki zao,kijamii kiuchumi na kisiasa
Katia maadhimisho hayo yalipambwa na burudani mbali mbali za michezo iliyoandaliwa na wazee wenyewe sambamba na upimaji wa magonjwa ambayo yanaonekana kuwasumbua wazee ambayo ni kisukari na shinikizo la damu.
Imeandikwa na Jacquelen Clavery
Afisa Habari Songea DC
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa