Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Songea Mhe, Simon Kapinga amewahasa madiwani kuwahamasisha Wazani kwa kushirikiana na viongozi wa kata vijiji na Tarafa, kuendelea kushirikiana katika kuhakikisha kila mototo aliye na umri wa kwenda Shule apelekwa shukeni
Mhe. Kapinga ameyasema hayo wakati anahitimisha Kikao cha robo ya pili cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri 31st January 2024
“ kwa wale wanafunzi ambao hawajaripot mashuleni, Shule zishafunguliwa na kunawanafunzi wamefaulu masomo yao ya kujiunga na kidato cha kwanza ila mpaka sasa hawajaripoti mashuleni, tunazo nguvu za watendaji wa kata wakishirikiana na wazazi tuhakikishe watoto wananenda Mashuleni”. Saimon Kapinga
Aidha makam mwenyekiti wa Halmashauri ya Songea ambae pia ndie aliyeongoz a Baraza la madiwani la 31st January 2024, Mhe, Simon Kapinga amewahasa madiwani kuwahamasisha wananchi kulima zao la ufuta kwa wingi kwani ni zao ambalo lina mpa mkulima fedha ya mapema sana na kuondokana na matatizo ya kiuchumi.
"Niwahase madiwani wenzangu mhakikishe mnawahamasisha wananchi walime zao la ufuta hasa kwa kipindi hiki cha mwezi huu wa pili kwasababu ni zao linalo wapatia hela mapema na kuwasaidia katika majukumu mengine"
Amesisitiza Kapinga
Hata hivyo Mhe. Mwenyekiti amewataka watendaji wa kata kuhakikisha wanawahimiza wazazi na walezi kuwasimamia watoto katika masomo na sio kuwaacha wajiingize kwenye ajira ambazo zimekuwa zikiharibu ratiba za masomo yao
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa