Mkutano wa Baraza la Madiwani robo ya pili Octoba hadi Desemba 2024/2025 uliofanyika leo 31/01/2025 katika Ukumbi wa Lundusi, Halmashauri ya Wilaya ya Songea, umewathibitisha Watumishi watatu kuwa wakuu wa Disheni na Vitengo.
Wakuu hao wamethibitishwa na Baraza lilioongozwa na Makamu Mwenyeki wa Halmashauri Mhe. Simon Kapinga na kushuhudiwa na Wageni Mbalimbali akiwemo Mwenyekiti na Katibu wa CCM Wilaya ya Songea, na Kaimu Katiba tawala Mkoa wa Ruvuma Bi Amina Tindwa na wagen wengine.
Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Simon Kapinga amesema
“Kwakua wameshamaliza muda wao wamatazamio naomba kuwathibitisha wakuu wa divisheni na vitengo kwa mujibu wa kanuni ya 14 ya utumish wa umma ya mwaka 2020.
Akiwataja wakuu hao Mhe kapinga alisema
“Watumishi walithibitishwa leo ni pamoja na Geofrey Romanus Kihaule, Mkuu wa Divisheni ya Huduma za Afya Ustawi na Lishe, John Rafael Luoga Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA na Paschal Odo Kapinga Mkuu wa Kitengo cha huduma ya Sheria
Mkutano huo pamoja na mambo mengine umepokea taarifa kutoka kamati mbalimbali za kudumu za Halmashauri kama vile Kamati ya Maadili, kamati ya kudhibiti Ukimwi, Kamati ya Uchumi ujenzi na Mazingira pamoja na Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa