Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Peramiho Simoni Bulenganija amewataka wasimamizi wa uchaguzi mkuu ambao ni wakuwachagua Madiwani ,Wabunge na Rais kuheshimu na kuthamini zoezi la uchaguzi kwa sababu wasimamizi ni kundi la mwisho katika kufanikisha uchaguzi kwa kushirikiana na wasimamizi ngazi ya Jimbo na kata
Bulenganija ametoa kauli hiyo leo kwa nyakati tofauti wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa wasimamizi wa uchaguzi mkuu,yaliyofanyika katika Mji mdogo wa Peramiho na Kijiji cha Mpitimbi katika Jimbo la Peramiho Mkoani Ruvuma.
Bulenganija amesema uchaguzi ni swala la Kikatiba,sheria ,taratibu na kanuni ,hivyo nivema wasimamizi wakafikiria kwa umakini na busara katika kufanikisha kazi hiyo na kuzingatia na maelekezo na maagizo mbalimbali yanayotolewa naTume ya Taifa ya Uchaguzi na kutofanya makosa katika kufanikisha zoezi hilo.
“Nisingependa kusikia mtu amechelewa kufika katika kituo chake na kuchelewesha zoezi kuanza”,amesema Bulenganija.
Amesema uzembe,au kujitoa ufahamu katika kufanikisha uchaguzi ni vitendo ambavyo havikubaliki kila usimamizi anatakiwa kujiamini na kujitambua ili aweze kutimiza majukumu yake kwa uweledi mkubwa pia kuacha tabia ya kufanya kazi kwa mazoea kwasababu yanaweza kusabisha dosari na kasoro.
Jimbo la uchaguzi la peramiho linavituo 252 vya kupigia kura, kila kituo kitakuwa na watendaji wanne na jumla ya watendaji wote kuwa ni 1,008 ambao wote wamepata mafunzo na kula kiapo cha kutunza siri na chakujivua uachama
Imeandikwa na
Jacquelen Clavery
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa