Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, wamesogezewa huduma katika eneo lao, ili waweze kupata Hati ya kumiliki viwanja pia kupata utatuzi wa migogogro ya Ardhi ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Huduma hii itakayodumu kwa siku tatu, yaan Jumanne, Jumatano na Ijumaa imekua msaada sana kwa wakazi wa jimbo la Peramiho na kata zake. Zoezi la kusikiliza malalamiko ya wananchi kuusu masuala mbalimbali yanahusiana na viwanja pamoja na umiliki, limekua likifanyika, lakin kwa sasa limeboreshwa, ili kuhakikisha kero hii inakwishwa kwa asilimia zote.
Akizungumza Kamishna msaidizi wa Ardhi mkoa wa Ruvuma Ngd. Saidi Juma Kijiji amesema “ leo tupo kwenye zoezi letu la kawaida, zoezi la kusikiliza malalamiko kwa wananchi. Tumejiwekea utaratibu huu baada ya Mhe. Waziri kutoa maelekezo ya siku miamoja ya kushughulikia malalamiko yote yanayohusiana na maswala ya Ardhi. Tulianza wiki iliyopita katika manispaa ya Songea, lakin leo tupo Halmashauri ya Songea na tutakuwepo kwa siku tatu”
“Zoezi kubwa ni; moja kushughulikikia malalamiko yote yanayohusiana na ardhi kwenye Halmashauri ya Songea lakini pili ni kutoa Hati za papo kwa papo kumbuka sekta za ardhi zote zipo hapa kwaajili ya kushughulikia na shughuli mbalimbali au changamoto mbalimbali zinazohusiana na maswala ya Ardhi”
“Maelekezo aliyoyatoa Mhe. Waziri ni pamoja na utoaji wa Hati kwa wakati, na ikumbukwe pia gharama za upatikanajini wa Hati zimepungua ambapo ukiwa na shilingi elfu hamsini unaweza kupata Hati kwa kiwanja kimoja, ambayo ni nusu ya gharama za awali”.
Aidha ofisi ya msajili wa hati, ni miongoni mwa ofisi zilizofika Halmashauri ya Songea lengo ikiwa ni kuhakikisha wananchi wanatambua umuhimu wa utunzaji wa nyaraka, pia namna ya kufanya kama umeuza ama umenunua kiwanja ili kuweka majina yako na kuepuka migogoro kwa baadae.
Christina Daniel Nyerere, Msajili wa Hati Msaidizi Mkoa wa Ruvuma anasema “ kunachangamoto mwananchi anaweza kuipata kama hatofanya miamala inayopatikana kwenye ofisi ya Msajili wa hati ikiwemo kwenye kubadilisha majina, ama umeuza kiwanja chako umemuamishia mtu mwingine, Yule mtu asipofanya mabadiliko kwa wakati itamgarimu kwanza, atakiendeleza bila kufanya mabadiliko kwa wakati itamgharimu kwanza atajikuta analipa gharama kubwa serikalini tofauti angefanya kwa wakati”
Dicksoni Emmanueli, ni mpima Ardhi wa Mkoa wa Ruvuma, kwa nafasi yake nae alikua na haya ya kusema “ leo tupo hapa kwa sababu, huu mji mdogo wa Peramio tulishapima viwanja zaidi ya 2300, lakini kabla ya hapo kulikua na viwanja 2000, pamoja na kupima lakini bado mwamko wa wananchi kuja kumilikishwa viwanja umekua mdogo sana, hivyo tunapokua na viwanja vingi vimepimwa lakini havijamilikishwa inakua haina faida ya upimaji, hivyo basi ili kuwasaidia wananchi wajue umuhimu wa kupimiwa ni lazima pia wawe na nyaraka”
“Si hilo tu, tumekuja kuwahamasisha wananchi kwakuwa hata gharama za upimaji zimepungua, mwaka jana walikua wanalipa laki moja na hamsini lakin kwa sasa ni shilingi elfu hamsini, hivyo mwananchi ambaye alipimiwa aje amilikishwe kwa sababu gharama zimeshushwa. Watu wasiendelee kujenga maeneo ambayo hayajapimwa”
“Hili ni zoezi la kimkakati, ikizingatia tuna mpango wa kutoa Hati miliki zaidi ya Mia Tatu (300) kwa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, ambalo linawekwa katika umuhimu wa kulinda umiliki pamoja na kuondoa migogoro. Tunaendelea kutoa wito kwamba zoezi hili ni endelevu na tutaendelea kufikia wananchi wote katika maeneo mbalimbali”. Alisem Saidy Mrisho Msananga, Afisa Ardhi Mteule Halmashauri ya Wilaya ya Songea
Wanachi wemeshukuru Serikali, Waziri pia mkoa na Halmashauri kwa kuwafikishia huduma hii karibu nao, namna wanavyotatiua migogoro inayohusiana na Ardhi pia kuwarahisishia namna ya kupata hati.
Theresia Msuya, mkazi wa kijiji cha Peramiho A, amesema “ tunashukuru sana hili zoezi linaloendelea kwani kwa upatikanaji wa Hati utanisaidia kwa mambo mengi sana, ikiwa ni pamoja na kupata Mkopo lakini pia inaweza kutumika kama dhamana. Zamani haikua rahisi hivi kilikua ni kitu kigumu sana kupata Hati, ila kwa sasa Serikari imerahisisha kwa kuleta kijijini kwetu. Nawashkuru viongozi wote wa wilaya, Mkoa Taifa kwa kuona wananchi wengi wanapata shida kupata hati na sasa wameturahisishia.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa