Wananchi wa kutoka kata mbalimbali za Halmashauri ya Wilaya ya Songea, wamejitokeza kuupokea Mwenge wa Uhuru uliofika leo Halmashauri ya Wilaya ya Songea na Kupokelewa katika Kijiji cha Lipaya kata ya Mpitimbi.
“ ni matumaini yang u kuwa, Wananchi waliohudhulia leo wapo tayari kuupokea Mwenge wa Uhuru, na sasa tupo tayari kuukimbiza Ee Mwenyezi Mungu tusaidie “ Kapenjama Ndile Mkuu wa Wilaya ya Songea
Mwenge wa uhuru umeingia Halmashuri ya Wilaya ya Songea ukitokea Wilaya ya Namtumbo. Mwenge umekimbizwa umbali wa kilometa 78.4 na kukagua miradi mbalimbali.
Katika Miradi hiyo, Miradi 3 imewekwa jiwe la Msingi, Miradi miwili imezinduliwa na miradi 4 imetembelewa, yote ikiwa na thamani ya Shilingi billion nne na million miatano.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi wa wananchi wamemshkuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani pamoja Mbunge wa Jimbo la Peramiho kwa Nman ambavyo wamekuwa wakiwaona wananchi wa jimbo la Peramiho kwa kuwaletea Miradi katika maeneo yao miradi ambayo imekuwa ikiwaokoa sana na kurahisisha maisha yao.
“ mimi nimshukuru sana Rais, kama asingetuona hata huu mwenge usingefika huku. Leo tunauona Mwenge kwakua tunayo Miradi ambayo unaweza zinduliwa na kwa ujio wa Mwenye miradi imeanza kufanya kazi mfani Mradi wa Maji leo tumeona maji yakitoka” Salimu Nyoni Mkazi wa kijiji cha Lipaya
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Songea, Mhe. Kapenjama Ndile amewashukuru sana wananchi waliojitokeza katika kukimbiza Mwenge huo ulioingia Halmashauri ya Wilaya ya Songea leo. Naye kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa amewataka wananchi kuendelea kumtia moyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani kwani nia yake kwa wananchi ni kuhakikisha wanamapata mahitaji yote muhimu kama vile maji, Miundombinu kama shule hospitari nk
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa