Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma wameanza kunufaika na uvunaji wa mazao ya misitu ya asili kwa kuchana mbao na mazao yake.
Akizungumza kwaniaba ya Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Ndongosi Omari Nassoro amesema wameanza kupata mafanikio baada ya kupewa mafunzo na taratibu za kuhifadhi misitu ya asili kutoka kwenye Program ya kuboresha mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu (FORVAC).
Nassoro amesema licha ya kupatiwa mafunzo hayo FORVAC imewasaidi mashine ya kisasa kwaajili yakuchana mbao ambayo wanaitumia katika kazi hiyo kwa uangalizi na usimamizi wa Halmashauri.
Naye Mwenyekiti wa kamati ya mali asili wa Kijiji cha Ndongosi Lukas Banda amesema katika kuhakikisha msitu huo unabaki salama kamati imegawana majukumu ya kulinda msitu kwakufanya doria kwania ya kuwabaini waharibifu wa misitu na kuwachukulia hatua wanaobainika.
Banda amesema pamoja na kunufaika na uvunaji wa misitu hiyo misitu hiyo wananufaika nayo kwakufuga nyuki na kuvuna asali.
Kwaupande wake Afisa Misitu wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Zakayo Kaunda amesema miti inayotakiwa kuvunwa ni yenye ukubwa wa sintimeta 45 na kuendelea.
Halmashauriya Wilaya ya Songea inajumla ya misitu ya hifadhi 11 kati ya misitu hiyo misitu mitatu ambayo misitu ya Lihiga, Mitumbati na Lupagalo wananchi wameanza kunufaika nayo kwa kuvuna mazao ya misitu.
Imeandaliwa na kuandikwa na
Jacquelen Clavery.
Songea DC.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa