Wananchi wa kata ya Magagura na wadau mbalimbali wa maendeleo wa Halmashauri ya Wilaya Songea mkoani Ruvuma wameunga mkono jitihada za mbunge kwakuchanga fedha ambazo zimetumika kunua vifaa tiba vya kituo cha afya cha Magagura na zawadi kwa wenye uhitaji.
Vifaa vivyo vimekabidhiwa katika sherehe za uzinduzi wa siku ya wanawake dunia iliyofanyika katika Kata ya Magagura,Kijiji cha Magagura hivi karibuni.
Diwani wa Kata ya Magagura Mhe.George Ponera amesema katika kuadhimisha siku hiyo wananchi wa kata hiyo wamechanga shilingi 690,000,ambazo zimetumika kunulia vifaa tiba,wadau wengi ambao wameshiriki kuunga mkono jitihada hizo kuwa ni Chuo cha Maendeleo ya Jamii cha Mlale ambacho kimechangia shilingi milioni tano na baadhi ya fedha hizo zimetumika kunua kitanda kwa ajili ya kujifungulia akinamama kiti kimoja cha kutembelea wagonjwa na vifaa tiba.
Mhe.Ponera amewataja wadau wengine kuwa ni Kikosi cha JKT Mlale ambacho nacho kimechangia vifaa tiba,Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo imechangia vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi 800 000 na Banki ya NMB ambayo imechangia shuka 12 kwa ajili ya wagonjwa zenye thamani ya shilingi 520,000 na kitanda kimoja kwa ajili ya kujifungulia akinamama ambacho thamani yake bado haijajulikana.
Mhe.Ponera amewashukuru wadau mbalimbali waliojitokeza kuchangia vifaa hivyo na fedha ambazo zinakwenda kupunguza tatizo la upungufu wa vifaa tiba katika Kituo cha Afya cha Magagura na wananchi wa Kata hiyo na Kata jirani kuweza kunufaika na huduma za afya.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bi Lucy Mbolu amesma katika kuunga mkono jitihada hizo Halmashauri imetoa kiasi cha shilingi milioni 15 ambazozitatumika kakarabati miundombinu ya umeme na kurekebisha miundombinu ya mifumo ya maji.
Akimwakilisha mgeni rasmi Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Menas Komba amesema katika kuadhimisha sherehe za wanawake duniani Mhe.Jenista Mhagama ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Peramiho ametoa shilingi milioni 2,200,000 kwa ajili ya kununulia vitanda na magodoro yake ambavyo vitatumika kwa wagonjwa watakao takiwa kupumzishwa pia ametoa shilingi milioni tano kutoka kwenye mfuko wa Jimbo kwa ajili ya kwenda kujenga miundombinu ya elimu katika shule ya Msingi Mlale.
Mhe.Komba ameongezakwakusema maadhisho ya siku ya wanawake duniani yaendane na matendo ya halisi ya kuthamini mchango wa wanawake katika jamii ikiwemo utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa makundi ya wanawake,vijana na wenye ulemavu.
Kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani Halmashauri ya wilaya ya songea imefanya uzinduzi wa sherehe hiyo katika kijiji cha Magagura ,kata ya Magagura kwakufanya matendo ya huruma kwakugawa zawadi kwa wahitaji kwa wanawake toka Kata ya Mpandangindo na watoto yatima wanaolelewa na Shilika la Masista wa Mtakatifu Agnes Chipole.
Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani hufanyika kila mwaka Machi 8 kuanzia mwaka 1975 ikiwa na maudhui ya kutambua na kuthamini mchango wa wanawake katika jamii na kuikumbusha dunia juu ya haki za wanawake na kuongeza chachu katika harakati za mapambano katika usawa wa kijinsia kwenye jamii kwa mujibu wa” UMOJA WA TAIFA”
Imeandaliwa na kuandikwa na
Jacquelen Clavery
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa