Wafugaji watakiwa kusomesha watoto
Katika Kaya 248 za jamii za wafugaji katika kijij cha Mhepa kata ya Kilagano Halmashauri ya Wilaya ya Songaea kaya 3 tu zimepeleka watoto wao shule na wasiozidi 10
Mkuu wa Wilaya ya Songea Mh Pololeti Mgema amebainisha hayo wakati wa uzinduzi wasoko la awali wa mnada wa mifugo ulio fanyika kijiji hapo hivi karibuni.
Ameshangazwa na hali hiyo kwa jamii za wafugaji katika kaya 248 kaya 3 tu zinasomesha watoto tena wasiozidi kumi wakiwemo Wabarbeig na wasukuma.
Mh Mgema amesema jamii za wafugaji walio wengi hawependi kusomesha watoto,kwa lengo la kuwarithisha shughuli ya ufugaji, na kuwakosesha haki yao ya kikatiba ya kupata Elimu
Kufuatia hali hiyo ametoa agizo kwa jamii za wafugaji wa Kijiji hicho kuwapeleka watoto shuleni mara moja wakapate Elimu,atachukua hatua kali za kisheria kwa mfugaji yeyote atakaye kaidi agizo hilo la kuto somesha wototo.Elimu inatoa fursa kwa watoto katika kujijengea misingi bora ya maisha katika kupanga na kutekealeza kazi zao.
Wafugaji wamesema wanashindwa kuwa peleka watoto wao shule kutokana na changamoto ya umbali uliopo kati yao na shule ilipo na wameomba serikali kuwatengea eneo la kujenga shule nao wapo tayari kuanza ujenzi ili watoto wao waweze kusoma.
Aidha uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea umesema upotayari kuwa pelekea watumishi endapo watakamilisha ujenzi wa shule.
JACQUELEN CLAVERY –TEHEMA.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa