Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Bi Elizabeth Gumbo, anasema utoaji wa Mikopo ya asilimia 10/% kwa Vijana, Wanawake na Watu wenye ulemavu, vikundi 50 mpaka sasa vishapata mikopo
Bi Elizabeth amesema katika Halmashauri hiyo Kwa mwezi Jan, 2025 wamefanikiwa kutoa mikopo zaidi ya shilingi milioni 500 kwa Vikundi 50 vya wajasiriamali kati ya 100 walioomba.
Mkurugenz Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, ameyasema hayo hii jana Jan 15,2025 akizungumza kupitia Selous FM kwenye kipindi Cha Kijiwe Cha Kahawa ambapo ameeleza mchakato wa utoaji wa Mikopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Songea ulianza tangu Mwezi Septemba, 2024 dirisha la Maombi lilifunguliwa.
Bi Gumbo ametoa pia tathmini ya zoezi la uboreshaji wa daftari lakudumu la mpigakura Hadi kufika sasa waliojitokeza kuboresha taarifa zao pamoja nakujiandikisha ni wastani wa asilimia 50% Vijana wanatajwa kujitokeza kwa wingi,kukiwa na vituo 230 vyakujiandikisha.
Aidha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Bi Elizabeth Gumbo amezungumzia kuhusu sekta ya Elimu akimshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha miundombinu ya elimu inaboreshwa, amesema katika wakati huu ambapo shule zimefunguliwa ni asilimia 75% ya wanafunzi wameripoti Shuleni ndani ya Halmashauri yake, ametumia nafasi hiyo kuwataka wazazi na walezi kuhakikisha mahudhurio ya wanafunzi yanaongezeka Shuleni.
Kuhusu utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayofikia zaidi ya 70 Hadi 80 anasema "ipo iliyokamilika, ipo iliyopo kwenye msingi lakini iliyo mingi imenyanyuka ".
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa