Halmashauri ya wilaya ya songea imezindua mnada wa awali wa soka la mifugo ambao utasaidi kuongeza pato laSerikali katika kijiji cha Mhepai Kata ya kilagano.
Mnada huo umezinduliwa na mkuu wa wilaya ya songea Mh Pololeti Mgema hivi karibuni.
Akizindua mnada huo Mh Pololeti amesema mnada ni fursa ya kiuchumi kwa serikali na kwa jamii kwa kupitia mnada,serikali itakasanya ushuru na jamii itanufaika kupiti huduma mbalimbali za biashara za kuuza mifugo na bidhaa mbalimbali.
Mh Pololeti amewataka wafugaji kufuga kulingana na wakati na kufanya shughuli nyingine za kiuchumi kavile kilimo,usafiri na usafirishaji kupitia mifugo yao kama mtaji wa kuanzia na kuachana na ufugaji wa mazoea ambao kwa sasa hauna tija kubwa kwao.
Wazo la kuanzisha mnada limetokana na uwepo wa mifugo mingi iliyokuwa inaingia kutoka nje ya Halmashauri ya Wilaya hali iliyowapelekea wafugaji kuhitaji huduma ya soko la manada wa mifugo ili waweze kuuza na kujipatia mahitaji mengine muhimu.
Mnada utahusisha mifugo yote wakiwemo kondoo,jingo la mnada lilijengwa mwaka 2008/ 2009 na kuanza kutoa huduma lakini baadae mwaka 2011 soko la mnada lilisima kutokana na changamoto za kimiundo mbinu.
Aidha soko la mnada litafanyika kila tarehe7 na 25 ya kila mmwezi baada ya kuzinduliwa tena.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa