Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea inayoongozwa na Mwenyekiti wa Halmashuri Mhe. Menas Komba imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea
Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Magima iliyoanza kujengwa kwa nguvu za wananchi hivyo serikali ikapeleka kiasi cha shilingi milioni 50 kwaajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa Zahanati hiyo na mpaka sasa kiasi kilichobaki ni shilingi 60,55,000 huku ujenzi ukiwa kwenye hatua za ukamilishaji.
Pia kamati hiyo iliendelea na ziara katika shule ya Msingi Parangu iliyoko Kijiji cha Parangu ambapo kamati ilikagua mradi wa SWASH matundu 15 ya vyoo ambapo shule hiyo ilipokea kiasi cha shilingi 37,643,862.66 kwaajili ya ujenzi wa matundu 15 ya vyoo na mpaka kamati hiyo inakagua mradi huo tayari umkwisha kamilika.
Kisha kamati ya Fedha ilielekea katika Kijiji cha Kilagano kitongoji cha Nambalapi na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na fedha za BOOST katika shule mpya ya mkondo mmoja shule ya Msingi Nambalapi ambapo katika shule hiyo ilipokea jumla ya shilingi 331,600,000 kwaajili ya ujenzi wa madarasa 7 ya Shule ya Msingi, vyoo, jengo la Madarasa mawili ya awali ya Mfano na jengo la utawala. Na mpaka kamati inafika kwenye mradi huo mradi upo kwenye hatua za ukamilishaji.
Ambapo katika taarifa iliyosomwa na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo mbele ya Mwenyekiti wa Halmashuri wameweza kumshukuru Mhe Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwatengea kiasi hicho cha fedha, pia wameshukuru, Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mhe Jenista Joakim Mhagama kwa namna anavyolipambania Jimbo lake, pia wamekishukuru Chama cha Mapinduzi kwa kutekeleza ilani ya Chama , pia wamemshukuru Mwenyekiti wa Halmashuri pamoja na baraza la Madiwani kwa kuona umuhimu wa ujenzi wa shule hiyo kwani wanafunnzi walikuwa wakisafiri umbali mrefu kwaajili ya kwenda kusoma jambo ambalo lilikuwa linahatarisha usalama wa wanafunnzi
Kisha Mwenyekiti wa Halmashuri ametoa wito kwa vijiji vyote vya Halmashauri ya Wilaya ya Songea kuhakikisha wanakuwa na akiba ya tofali ili kurahisisha ukamilishaji wa miradi pindi inapoelekezwa kwenye vijiji vyao kwani baadhi ya miradi imechelewa kukamilika kutokana na uhaba wa matofali katika vijiji husika
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa