Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Songea, inatarajia kuanza ujenzi wa Madarasa mawili ya Awali ya Mfano kupitia Mpango LANNES yenye thamani ya shilingi Milioni 57,825,000.00katika shule ya Msingi Ndilima, Ujenzi huo unatarajia kuanza rasmi tarehe 08/09/2023.
Awali kamati ya ujenzi wa mradi huo wameweza kukutana katika ofisi ya kata ya maposeni tarehe 05/09/2023 ikiongozwa na Mwakilishi wa Afisa Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mwl. Sothery Nchimbi ambaye ni Afisa Elimu Maalum idara ya Elimu Msingi ili kuzijengea uwezo Kamati za ujenzi kupitia Force Akaunti.
Ambapo katika maelezo yake Mwakilishi wa Afisa Elimu wa Msingi ambaye ni Afisa Elimu Maalum Halmashauri ya Wilaya ya Songea ameiomba Kamati ya ujenzi kuwa waaminifu na kushirikiana katika kufanikisha ujenzi wa Madarasa hayo.
" Tunafanya ujenzi kwa ajili ya kuwezesha watoto wetu na wajukuu wetu waweze kusoma katika mazingira mazuri kwa hiyo niwaombe ndugu wajumbe kufanya kutekeleza ujenzi huu kwa uaminifu na kwa kuzingatia ubora na kwa kuangalia mstabali wa maisha ya watoto wetu ambao ndio watakao soma katika Madarasa hayo na kwa kufanya hivyo tutakuwa tumetekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi katika uboreshaji Elimu ya Tanzania"
"Aidha namshukuru Mheshimiwa Rais, Daktari Samiah Suluhu Hassan Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha kwa ajili ujenzi wa miundo mbinu ya Elimu katika wilaya ya Songea Aidha nawashauri kamati kuepuke kufanya kazi kiurafiki kwani tutakwamisha ujenzi,na kusababisha kujenga chini ya kiwango au vinginevyo"
Pamoja na hayo Mwakilishi huyo wa Afisa Elimu alitoa nafasi kwa wataalamu kutoka ofisi ya Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ili kutoa ufafanuzi wa kitaalamu wa mambo yanayohusu ujenzi kwa lengo la kufanikisha ujenzi huo, Maafiasa hao walikua na haya ya kusema-;
Raymond Joseph Afisa Manunuzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea" Lengo la kushirikiana kamati hii pamoja na wajumbe tunahitaji kuweka uwazi wa mradi, lakini kama Afisa manunuzi nawashauri kamati ya mapokezi ya ujenzi huu kuwa na kitabu cha reja ambacho kitasaidia kuandika vifaa vyote vitakavyo nunuliwa sokoni na kutoka stoo kuelekea kwenye ujenzi ili kuepusha upotevu wa vifaa wakati wa ujenzi"
Sambamba na hilo ni vema tukapata bei za sokoni ili kuepuka gharama kubwa za vifaa vya ujenzi ambazo zitaweza kukwamisha ujenzi huu, tuepuke kununua vifaa kwa kufuata urafiki na tusisahau kutunza risiti za manunuzi ili kutunza kumbukumbu" Alisema Raymond Joseph, nae
Jacob Mchaki Mhandisi wa ujenzi na katibu wa kamati ya ujenzi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Songea Alisema "Ni muhimu kwa kamati ya ujenzi ikazingatia mambo yafuatayo ili kufanikisha ujenzi huu, kuainisha mahitaji ya ujenzi, kuandaa ripoti ya maendeleo ya mradi ( progress report),. Kupokea na kujadili taarifa ya kamati ya mapokezi na kupokea, kujadili na kufanyia kazi ushauri wa wadau mbalimbali". Pia
Emmables Francis Afisa mazingira kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Songea Alisema "Nilazima kuwepo kwa ushirikishwaji wa jamii juu ya mradi huu ili kuepusha migogoro hususani ya maeneo, pia kuzingatia eneo la upatikanaji wa nyenzo za ujenzi hususani kokoto na mchanga ili kuepusha uharibifu wa mazingira, kabla ujenzi haujaanza lazima kuwepo na choo kwaajili ya kuwezesha mafundi kujisitiri na haja, eneo la kuweka taka ngumu ili kuepusha utupaji wa taka hovyo na kupeleka uchafuzi wa mazingira, pia kutunza uoto wa asili na mwisho kuangalia ustahimilivu wa udongo kama unaweza kubeba jengo lenye kiwango gani.
Ikumbukwe kwamba mradi huu wa ujenzi upo chini ya ilani ya chama cha mapinduzi katika kuboresha Elimu ya Tanzania ambapo fedha za mradi zilikabidhiwa mnamo Tarehe 8 September 2022 na ujenzi huo unatarajiwa utaanza mara moja baada ya kikao hiki.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa