Maandalizi ya awali ya ujenzi wa kituo cha Afya Muhukuru yanaendelea vizuri na yamekamilika kwa asilimia 15 pamoja na uchimbaji wa msingi
Hayo yamesemwa na Mwandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Bw. Frank Hossea kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Songea Bw Simon Bulenganija, wakati akitoa ufafanuzi kuhusu maendeleo ya ujenzi kwa baadhi ya wanakamati ya ujenzi waliotembelea katika kituo hicho kwa lengo la kuangalia shughuli za ujezi zinavyo endelea hivi karibuni.
Bw Hossea amesema maandalizi ya awali yamekamilika kwa asilimia 15 pamoja na uchimbaji wa msingi kwa majengo yote matano ambayo yanatakiwa kujengwa, ununuzi wa vifaa vya viwandani kama vile Bati,Simenti na Nondo pamoja na ufyatuaji wa tofari ambao unaendelea.
Halmashauri ya wilaya ya songea imepata shilingi milioni miatano (500) kutoka OR-TAMISEMI-AFYA kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya Muhukuru ujenzi unaotarajia kukamilika miezi ya hivi karibuni
Kamati imeridhishwa na maendeleo ya ujenzi unavyo endelea na kutoa wito kwa watalamu kuwa makini kusimamia na kuharakisha ukamilishaji wa ujenzi huo.
JACQUELEN CLAVERY-TEHAMA
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa