TARURA na Mikakati ya kujenga, kuboresha miundombinu ya Barabara Halmashauri ya Wilaya ya Songea
Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) imeanza ujenzi,uboresha na kuimarisha miundo mbinu ya barabara katika halmashauri ya Wilaya yaSongea kwa lengo la kurahisisha mawasiliano na kukuza uchumi wa nchi.
TARURA imepanga kuhakikisha kuwa dhima ya serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli inayafikia malengo yake ya kuwa na Tanzania yenye uchumi wa kati pamoja na maendeleo ya viwanda.
Kaimu meneja wa TARURA Mwandisi Simoni Binanamu Amebainisha kuwa, miundombinu ya barabara katika halmashauri ya Songea zitajengwa,na kufanyiwa matengenezo ya muda maalumu na kawaida kwa lengo lakufanikisha shughuli za mawasiliano ya barabara kwakusafirisha mazao ya wakulima na kuboresha maisha ya wananchi.
Mwandisi Binamu alisema kuwa mpaka sasa kampuni tatu za wakandarasi zimesaini mikataba kwa ajili ya kutekeleza ujenzi na ukarabati wa miradi ya barabara katika Halmashauri ya Songea.
Serikari imetoa zaidi ya Shilingi milioni 692 kutoka mfuko wa barabara kwa ajili ya kufanikisha ujenzi huo ambapo kampuni za Ugalla Investment Company, Msae General Suppliers Ltd na Msifaki engineering and enterprises zimepewa tenda ya kufanya kazi hiyo,kwa muda wamiezi mitatu kuanzia machi 26 hadi Julai 27- 2018 ujenzi uwe umekamika
“Kampuni ya Ugalla Investment itafungua barabara mpya kuanzi Liganga-,Serekano-,Mborongo hadi Mwimbasi pamoja na ujenzi wa miundao mbinu kama vivuko na mifereji yenye urefu wa kilomita 30. Ambapo Msae General Entreprises atafanyia matengenezo ya kawaida na muda maalumu barabara za Peramiho-Morogoro-Litisha-Liganga.Peramiho-Litowa.Muunganozomba-Lugagara na Mgazini hadi Mhepai zenye kilomita 58.
Binamu aliongeza kuwa kampuni ya Msifaki Engineering and Enterprises imepewa barabara yenye kilomita 40 inayoanzia Matomondo, Magagula hadi Kizuka na barabara nyingine itaanzia Litapwasi, Lyangweni hadi Mbingamwalule.na Mahiro –Mpingi hadi Kikunja.Barabara zote zita jengwa kwa kiwango cha ngarawe
Kukamilika kwa barara hizo kutadhihirisha wazi utendaji mzuri wa kazi wa serikali ya awamu ya tano kwa leta mabadilikochanya kwa wananchi wake kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni na kuhakikisha pato la serikali linaongezeka na wananchi kuendelea kupata huduma bora za kijamii kama vile maji,madawa,Elimu nk.
IMEANDALIWANA. JACQUELEN CLAVERY –HABARI MAWASILIANO NA UHUSIANO SERIKALINI
HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA.
Halmashauri ya Wilaya Songea
Anuani ya Posta: P.o.box 995, Songea
Simu: 2602320 / 2602176
Simu ya mkononi:
Barua pepe: dedsongea@songeadc.go.tz
Copyright ©2017 songeadc.go.tz. Haki imehifadhiwa